Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 13, 2019

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda Amuomba Msamaha Rais Magufuli.....Amtaka Awahurumie ili Nao Watoke Kifungoni

juu
Wakati Rais John Magufuli akieleza sababu zinazomzuia kukutana na wanasiasa, viongozi wa vyama vya upinzani wamemtaka asiwe na hofu kukutana nao na kwamba pengine mtu aliyetishia kumchinja, alikuwa na maana ya “kuchinjwa kisiasa”.

Akizungumzia ushauri uliotolewa na Askofu Zachary Kakobe wa Kanisa la FGBF kutaka wanasiasa wakutane kama walivyofanya viongozi wa kidini, Rais alisema amekuwa akisita kwa sababu baadhi ya wanasiasa wanamtukana na wengine wametishia kumchinja na kumtupa baharini ndio maana ameamua awaache peke yao. Hata hivyo, alisema yuko tayari kukutana nao.

Hayo yalitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa mapokezi ya ndege mpya ya Serikali aina ya Airbus A220-300, ambako viongozi kadhaa wa kidini walipewa nafasi ya kufanya sala, akiwemo Askofu Kakobe, ambaye kabla ya sala aliomba aseme neno.

“Nimeusikia wito wa Mzee Kakobe kuwa walipokutana na wao (viongozi wa dini) kule, basi na sisi wanasiasa tuwe tunakutana,” alisema Rais.

“Mimi nimekubali sana, lakini tatizo ni kuwa huwezi kukutana na mtu anayekutana na kukuambia siku uchinjwe, utupwe baharini. Je, siku ukikutana naye iwe ndiyo siku ya kuchinjwa?”

Kauli hiyo ilimfanya mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda aombe radhi kama kiongozi wa wadau wa siasa na kwa niaba ya vyama vyote iwapo kuna kauli zimewahi kutolewa zenye mbomoko wa maadili.

“Nampongeza kwa kutambulisha utashi wake wa kutaka kukutana na viongozi wa vyama vya siasa. Hivyo kama kuna kauli ambayo imewahi kumkwaza atusamehe sisi wadau wa siasa kama ambavyo amekuwa akisamehe wafungwa ili na sisi tutoke kifungoni. Adhabu ya miaka mitatu inatosha,” alisema.

Alisema Rais anapaswa kuwapangia fursa ya kukutana nao ili awaeleze hisia zake na wao waeleze zao ili kudumisha utamaduni mzuri wa siasa kwa kuwa Tanzania ina deni la kuwa kielelezo cha siasa bora ya demokrasia ya vyama vingi.

Naye mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia alisema bado msimamo wake ni meza ya mazungumzo na kwamba hata alipokutana na Rais Ikulu, Novemba 13 mwaka jana alimsisitiza jambo hilo.

“Kauli ya mtu mmoja asiichukulie vibaya. Anatakiwa kujua kuwa yeye ni jalala,” alisema mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi akirejea msemo maarufu wa “ukubwa ni jalala”.

“Awe na moyo wa uvumilivu, aweke kipaumbele cha taifa mbele kwa kuwa nchi ni kubwa zaidi ya mtu yeyote.”

Alisema Watanzania wote wanapaswa kutunza nguzo ya hekima, umoja na amani kwa kuwa jamii yoyote yenye migogoro haiwezi kustawi.

Mbatia alitoa mfano wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga ambao siku za hivi karibuni walishikana mikono kumaliza tofauti zao na wamekuwa wakionekana pamoja katika shughuli za kitaifa, kijamii na kiserikali.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )