Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 24, 2019

PICHA: Basi la Fikoshi Lapinduka na Kuua Watu Wanne....42 Wajeruhiwa

juu
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya FIKOSHI linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Mwanza kupoteza mwelekeo na kupinduka katika eneo la Uvinza mkoani Kigoma usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa basi hilo, na kusababisha kupinduka.

“Ajali imetokea  maeneo ya Uvinza, kuna sehemu inaitwa Mnarani, ni barabara ya Vumbi, ilipofika maeno hayo ambayo ina kona kona nyingi, kwa mujibu wa mashuhuda wamesema dereva alikuwa kwenye mwendo kasi, alipofika maeno hayo, gari ikapinduka na kusababisha vifo vyo watu wanne wanaume watatu na mwanamke mmoja, na majeruhi 42.
 
"Majeruhi tumewachukua kuwapeleka hospitali ya Maweni ya Mkoa ambako wanaendelea kupata matibabu”, amesema Kamanda Otieno.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )