Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 17, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 55

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 

“Ethan kuna zawadi na kazi ambayo na sisi tuna hitaji utusaidie kuifanya”
Qeen alizungumza kwa sauti nyororo huku macho yakiwa yamemlegea kwa pombe nyingi aliyo kunywa, wakasimama na kunishika mikono yangu, nikatembea nao hatua chache hadi kitandani, kisha wakanisukumia kitandani, wakatazamana kisha wakacheka kidogo. Taratibu wakaanza kunnyana ndm zao huku wakianza kuvuana nguo zao jambo lililo nishangaza sana na kunitamanisha sana kihisia na kunifanya nipate msisimko mkali sana wakimahaba hadi nami nikajikuta nikianza kuvua nguo moja baada ya nyingine.

ENDELEA
Qeen na Latifa wakapanda kitandani huku wakiwa wamebakiwa na nguo zao za ndani. Kila mmoja akaanz akunipapasa mwilini mwangu jambo lililo nifanya nizidi kuchanganyikiwa, mlio wa simu yangu iliyomo kwenye suruali ambayo tayari nimeivua, ukatushtua sote. Latifa akanisogezea suruali yangu na kuitoa simu, nikaitazama kwa sekunde kadhaa namba ya Biyanka kisha nikaimnya kitufe cha kuzima simu hii na kuiweka pembeni.
 
“Sitaki usufumbufu”
Nilizungumza kwa sauti ya kilevi, nikaitumia simu pembeni na wasichana hawa wakaendelea na kazi hadi tukamalza huku wakishukuru.

“Mmmm, sipati picha jinsi unavyo fanya Biyanka”
Nikastuka kidogo Qeen kulitaja jina la Biyanka.
“Muna fahamu kwamba mimi na Biyanka tuna mahusiano?”
“Ndio ofisi nzima ina fahamu kwamba tuna muna mahusiano kwa maana ana tuchimba biti za chini chini kwamba hakuna mtu anaruhusiwa kukusogelea na kama kuna mtu mwenye shida na wewe basi ipitie kwake kisha yeye ndio anaileta kwako”
 
Nikazidi kushanga kwa vituko anavyo vifanya Biyanka pasipo kujua  nina mtumia kama silaha ya maangamizi kwa baba yake.
“Anacho kifanya sio kitu sahihi kwa maana mimi sifahamu kabisa”
“Ohoo sisi wa chini mkurugenzi ndio tunao jua hilo, hususani sisi wasichana warembo warembo ndio tunakoma kwa kupigwa mikrwa na inafikia hatua ameahidi akigundua kwamba kuna msichana ana mahusiano na wewe basi anamfukuza kazi”
 
“Heee huko kafika mbali kampuni ni yangu na asinipangie masharti kwa wafanyakazi wangu”
“Qeen unajua tatizo la Biyanka hajiamini, japo ni mzuri ila anaona atazidiwa kete na sisi watoto wa Kiswahili ndio maana kila asubuhi anaitisha vikao vya wasichana wote ofisini na kuwapa onyo”
 
“Nitamkanya kwa jambo hilo”
“Hapana Ethan, kusema kweli sisi tunaipenda kazi yetu. Najua huko kitandani atakudadisi kujua ni nani aliye kuambia, na utajikuta unatutaja, akatutumbua”
“Hamuniamini?”
Niliwauliza Qeen na Latifa kwa msisitizo.
“Tunakuamini”
“Sasa wasiwasi wa nini, mimi ninao uwezo pia wa kumfukuzisha kazi”
“Hee huko ni mbali sasa Ethan, usije ukafungiwa na baba yake, kumbuka kwamba anakwenda kuwa raisi wa hii nchi na ana washabiki wengi sana na kumbuka na chama chake ndio tawala hapa Tanania”
 
Nikakaa kimya huku nikiyatafakari maneno ya Qeen.
“Baba yake kuwa raisi anaweza kunifungia ehee?”
“Ndio, wanaweza kukufanyia figisu figisu hadi ukakuta unaitaifisha kampuni. Wanaweza kukufufulia madeni ya nyuma ya kodi hadi wewe mwenyewe ukajikuta unachanganyikiwa.”
“Ahaa….je asipo ingia madarakani itakuwaje?”
“Ni ngumu aisee ujue upinzani bado hawana uwezo wa kuking’oa chama pinzani madarakani”
 
“Kwa nini?”
“Moja hawana pesa za kutosha kama chama kilicho madarakani.Pili chama pinzani, vina wafuasi wengi mijini tu, ila huko vijijini ni hata havijafika, , ina mikoa mingapi, ina vijiji vipapi na kila kijiji kina wananchi wangapi wanao weza kupiga kura, sasa utakuta mwisho chama kilichopo madarakani, kinajichukulia ushindi mkubwa, upinzani wanabaki wana bwela bwela tu, wakidai wanaibiwa kura”
Latifa alizungumza kwa msisitizo.
“Hivi bado wana ibiana kura kweli?”
“Kuibiana ni kwenye kura labda za Ubunge na udiwani, ila kura za raisi ni mara chache kwa maana hapo watu wanapakodolea macho kishenzi”
 
“Mmmm nyinyi mupo chama gani sass?”
“Mimi sina chama kwa kweli, raisi atakaye patikana ndio huyo huyo.”
“Qeen je na wewe huna chama?”
“Mimi siasa za Afrika wala sizielewagi, unakwenda kupigwa na jua. Unampa mwenzako kura, ila mwisho anakuja kufanya yake serikalini, yaani hapo ndipo ninapo jikuta ninachoka kabisa.”
Maswali yangu ya udadisi yakazidi kunipa njia na mwanya wa kujua ni kitu gani ambacho ninaweza kukifanya. Kutokana baba Camila amesha pata kiti cha uraisi nina imani kwamba kwangu itakuwa ni njia rahisi kuhakikisha kwamba ananipa msaada mkubwa wa kukitoa chama  madarakani ambacho kwa sasa kimemsimamisha Poul Mkumbo.
 
“Muna fahamiana na kiongozi yoyote wa kipinzani?”
“Mmmm mimi sifahamu”
Qeen alizungumza huku akitingisha kichwa chake.
“Mimi nina mjua mmoja wao ila sidhani kama ana nguvu kubwa ndani ya upinzani”
“Ni nini unaye mfahamu?”
“Mbunge wa Arsha mjini, amemuoa dada yangu, mtoto wa mama mkubwa”
“Ahaa unaweza kuwasiliana naye”
“Sasa hivi?”
 
“Ndio ikiwezekana”
“Alafu nina muambiaje?”
“Utanipa mimi niweze kuzungumza naye”
“Ngoja nitazame”
Latifa akashuka kitandani, akachukua pochi yake kwenye moja ya sofa na kutoa simu yake, akaanza kuiminya minya na kuiweka sikioni mwake.
“Inaita”
Latifa alizungumza huku akirudi kitandani.
“Shem shikamoo”
“Samahani mwaya nitakuwa nimekusumbua”
“Sasa shemeji kuna bosi wangu mmoja hivi anahitaji kuzungumza na wewe, sijui upo tayari kuzungumza naye”
Latifa akanikabidhi simu yake na nikaiweka sikioni mwake.
“Habari yako ndugu”
 
“Salama tu, naona mazungumzo ya kwenye sio mazuri sana. Sijui tunaweza kuonana”
“Hujanitambulisha jina lako ndugu yangu”
“Ni mmiliki wa kampuni anayo fanyia kazi shemeji yako.”
“Ohoo muheshimiwa Ethan”
“Ndio ni mimi, samahani tunaweza kuonana”
“Ndio niambie mulipo mimi ninaweza kufika”
“Upo Dar?”
“Hapana nipo Bagamoyo, nipo nina mapumziko mafupi”
“Ohhoo asante Mungu, mimi pia nipo Bagamoyo. Sasa huyu binti atakuelekeza sehemu nilipo”
 
Nikamrudishia Latifa simu yake na akamuelekeza shemeji yake katika hoteli tulipo kisha akakata simu. Nikashuka kitandani na kuwaomba tukaoge pamoja kwa maana tunatakiwa kuwa safi, tunapo kutana na mbunge huyu. Tulipo maliza kuoga kila mmoja akavaa vizuri kisha tukatoka ndani humu na moja kwa moja tukaelekea eneo kupatia vinywaji huku tukiwa tumekaa katika kigiza kidogo ili mradi watu wasiweze kuniona. Baada ya robo saa mbunge huyo akafika katika eneo tulipo huku akiwa ameongozana na mke wake. Tukasalimiana naye na Latifa akatutambulishalisha.
“Munaweza kutupisha tukazungumza kidogo”
Niliwaomba Latifa na wezake, wakatii nilicho waambia na wakasogea meza ya pembeni. 
 
“Niliomba kuweza kukutana na mmoja wa wana chama cha upinzani ili tuweze kujadilia mambo mawili matatu kwenye mbio za uchaguzi munazo zielekea.”
“Sawa sawa”
“Najua upinzani muna kiu ya kukitoa chama madarakani si ndio”
“Ndio ndio”
“Najua kitu kinacho waangusha sana ni pesa za kampeni si ndio?”
 
“Hujakosea kabisa muheshimiwa”
“Hadi sasa hivi ndani ya chama chako muna bajeti ya kiasi gani?”
“Mmmm baheti kuu ya kampeni ni bilioni mia tatu hamsini, huku chama cha wenzetu tunasikia wameandaa bajeti ya trilioni moja kwa ajili ya kampeni zao”
“Trilioni moja na Bilioni mia tatu ni mbali sana, wezenu wamewaacha kwa kiasi cha bilioni mia saba, mutazipata wapi hizo”
“Wao wanategemea pesa ili wapate kura ila sisi tutawaua majukwaani kwa maneno na sera zanye nguvu ambazo zitawashawishi wananchi kuhakikisha wana fanya maamuzi sahihi”
 
“Hilo ndio mulilo litarajia kwa sera za majukwaa mutoe chama kilichopo madarakani?”
“Ndio mkurugenzi”
“Inabidi muweze kuamka sasa, siasa haitaji maneno mengi. Siana ina hiji pesa, bila ya pesa ni kupiga porojo kwa maana wananchi hao munao wapa sera munazo dai ni nzuri, watahamia upande wa pili kusiliza sera huku wakikinga mikono kupata ridhiki ya chote kitu na mwishowe mutajikuta mukiwa munaangushwa kila chaguzi na mutaishi kulalamika weee na hakuna kitakacho tokea kwenu”
Bwana Samweli kama nilivyo tambulishwa na Latifa akaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akionekana kutafakari kile nilicho mueleza.
 
“Mimi nimeshirikia siasa nchini Ujerumani, wezenu kule upizani hawatumii kelele majukwaani, ni pesa ndio inafanya kazi. Watu wanataka chama chenye pesa kiwaongoze wao, sio chama masikini kama chenu kiwaongoze, kwa mfano tu mdogo muna pewa nchi mukiwa hamuna pesa, mutatumia kiasi gani kukijenga chama kwa pesa ya nchi?”
“Mmmmm hilo nalo neno”
“Ndio hivyo, mutakuta munaacha kuwashuhulikia wananchi shida zao, na munahamia katika kujenga chama ili miaka ijayo musitoke, na mutakuwa ni wezi kwa kuiba pesa za wananchi walala hoi”
“Ni kweli nimekuelewa mkuu, sasa unahitaji sisi tufanye nini?”
 
“Andaeni mkutano mdogo sana wa siri sana na viongozi wako wa ngazi za juu, kisha nijulisheni nije tukutane. Mukumbuke kwamba mimi ni mkwe mtarajiwa wa mgombea uraisi wa chama tawala. Hivyo muwe makini sana katika kila simu ambayo munanipigia na ikiwezekana musitumie namba zenu. Sitaki siku waje kuhack mazungumzo yangu na ikawa shida kwangu na kwenu. Mume nielewa?”
“Tumekuelewa mkuu nitahakikisha kwamba nina fanya hivyo haraka iwezekanavyo”
“Sawa nashukuru kwa muda wako. Tunaweza kuendelea kujumuika kwa pamoja kupata chakula cha usiku”
“Nashukuru sana ila tunaeleka kwa mama mkwe tuliweka ahadi ya kula nao chakula cha usiku”
“Ohoo vizuri sana, basi hakuna tabu” 
 
Nikaagana na bwana Samweli pamoja na mke wake na wakondoka katika eneo hili kisha mimi nikatangulia chumbani kwetu. Baada ya muda kidogo Qeen na Latifa nao wakaingia chumbani humu. Usiku huu hakika ni usiku war aha kwetu sote watatu, baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku, tukaendelea kupeana burudani hadi majira ya alfajiri ndio tukajipumzisha huku sote tukiwa tumechoka sana.
                                                                                                                ***
    Majira ya saa saba mchana tukaanza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha moyoni mwake kwani kile tulicho kifanya kusema kweli kimetuburudisha na kama ni weekend yetu basi imekwenda poa.
“Narudi jamani haya mahusiano yawe siri, sawa”
“Upo salama Ethan hatuto weza kufungua kinywa chetu kwa mtu yoyote”
“Sawa. Leo usiku nitaandaa mpango mzima wa nyinyi kuweza kufanya katika kazi ambayo nimewajulisha, kesho asubuhi ofisini kwangu nikipata muda nita waita niweze kuwaeleza kila mbinu tunayo paswa kuweza kuifanya sawa”
“Sawa mkuu”
 
Tukafika eneo linalo itwa Mbezi Beach wakaniomba niweze kuwashusha. Nikampa kila mmoja wao milioni mbili za Kitanzania, kisha nikaendelea na safari yangu hadi katika hoteli niliyo pangisha.
“Nahitaji funguo”
Nilimuambia muhudumu wa hoteli hii huku nikimtazama usoni mwake.
“Ohooo samahani Mr Ethan, funguo ameichukua mke wako uliye mtambulisha hapa kwetu na hivi sasa yupo chumbani huko”
 
Nikastuka kidogo kwa maana jana nilimzimia simu Biyanka na hadi sasa hivi sijaiwasha. Nikaiwasha simu yangu, ndani ya sekunde kadhaa ikaanza kuingia mfululizo wa meseji kutoka kwa Biyanka pamoja na mkuu wapolisi. Nikaanza kupitia meseji moja baada ya nyinngine za Biyanka na zote zinaonyesha malalamiko ya kwa nini sipatikani hewani. Nikaingia kwenye lifti na kupandisha gorofani, nikatembea kwa hatua kadhaa kwenye hii kordo hadi sehemu ulipo mlango wa chumba changu. 

Nikagonga kidogo na ukafunguliwa. Biyanka akanipokea kwa sura iliyo jaa hasira sana, sikuhitaji kusemeshea kitu cha aina yoyote zaidi ya kuingia ndani. Nikavua koti langu na kulirusha kwenye kiti.
“Umetoka wapi na ulikuwa wapi na ulikuwa na unafanyaje na kwa nini ulinikatia simu kisha ukazima eheeee?”
 
Biyanka alizungumza kwa ukali sana ambao sikuujali, nikaka kwenye sofa na kuweka nne, nikailegeze vizuri tai yangu kisha nikapitia meseji za afande Kimaro. Nikajikuta nikinyanyuka huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana mara baada ya kusoma meseji ya Afande Kimaro akidai kwamba Clara haonekani hospitalini na askari wake wawili alio kuwa amewaacha waimarishe ulinzi wameuwawa usiku wa kuamkia leo.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )