Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 10, 2019

Atiwa Mbaroni Akidaiwa Kumuua mke Mwenza

juu
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Jenesia Jackob (29) mkazi wa Kalenge kijiji cha Lusenga  wilayani Biharamulo kwa kuhusishwa na kifo cha Joyce Jackson (18) ambaye alikuwa katika hatua za mwisho kuwa mke mwenza wake.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema jans Februari 9,2019 kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ndani ya nyumba ukiwa na majeraha kichwani na kuchomwa kwa kitu chenye ncha kali sehemu za siri.

Amehusisha mauaji hayo na wivu wa mapenzi na kudai kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa ambaye alikuwa anapinga mipango ya mume wake kumuoa Joyce  na kuwa mke mwenza wa Jenesia.

"Uchunguzi wa awali umebaini kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mke mkubwa, hakutaka marehemu aolewe na mume wake kama mke mwenzake, marehemu alivuja damu nyingi baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha," alisema Malimi.

Akifafanua mazingira ya kifo, amesema marehemu alitekeleza tukio hilo wakati mume wake Barushimana Mtondo alipokwenda kulala kwenye msiba wa jirani yao.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )