Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 22, 2019

CHADEMA Watoa Tamko Sugu Kukamatwa na Jeshi la Polisi

juu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo February 22 2019 wamewaita waandishi wa habari na kutoa kauli kuhusu Mbunge wao wa CHADEMA Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye alikamatwa jana na kauchiwa kwa dhamana Mkoani Mbeya baada ya kuzungumzia kuhusu vitambulisho vya wafanyabiashara akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu (CHADEMA) Zanzibar amesema hatua hiyo inalenga kumsumbua kiongozi ili asiweze kutekeleza majukumu yake ya kibunge.

"Sababu ya yote yanatokea ni wivu, kinachoendelea Mbeya Mjini kumsumbua Sugu na wengine ni kwanini Sugu anapendwa Mbeya, kwanini Sugu anapendwa na wapiga kura wake, mapenzi ya watu wa Mbeya hayawezi kuisha kwa Sugu kwenda polisi bali watazidi kumpenda", amesema  Salum Mwalimu.

 
Aidha, Mwalimu amedai kilichozungumzwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi katika mkutano wake jijini Mbeya hakukuwa na viashiria vyovyote vya ukiukwaji wa sheria.
 

Jana, Februari 21, 2019, Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya lilimshikilia Mbunge huyo  kujibu madai ya kutoa kauli ya uchochezi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC)  Urich Matei,  ni kwamba Sugu ameonekana katika moja ya clip za video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akisikiliza hoja na malalamiko ya wananchi na kuyatolea ufafanuzi na ndipo alipoongea kwa kutoa msimamo wake kuhusu zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo-wadogo (wamachinga) na kusema havifai na vinastahili kuchomwa moto.
 
Sugu alizungumzia suala hilo Februari 16, 2016 baada ya kutoa msaada wa saruji, nondo na mabati katika Shule ya Ikuti Mbeya ambapo aliwaahidi wananchi kuwa atakwenda kuhoji bungeni suala la vitambulisho wanavyouziwa ‘Wamachinga’ kwa bei ya shilingi 20,000/= ili kujua msingi wake na kwanini limeanza kufanyiwa kazi bila kuwashirikisha wadau ili kuwa na uelewa wa pamoja.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )