Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 6, 2019

Ilichokiamua Mahakama Kuhusu Kesi ya Utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu Takukuru

juu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kusikiliza kwa siku tatu mfululizo kesi ya Utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato chake, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru,Godfrey Gugai.

Wakili kutoka (TAKUKURU) Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba jana alisema kuwa kesi hiyo ilitakiwa kuendelea lakini wameshindwa kuleta mashahidi kutokana na kutokuwa na taarifa kama Hakimu amemaliza likizo.

Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa akaiomba Mahakama itoe ahirisho fupi ili dhamira ya kumaliza kesi hiyo ionekane kwani wateja wake wamekaa ndani kwa muda mrefu.

Baada ya Maelezo hayo Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuleta mashahidi tarehe itakayopangwa ili kesi hiyo ikamilike kwa wakati na washtakiwa waweze kujua hatma yao.Kesi hiyo imeairishwa hadi Februari 19,20 na 21, 2019.

Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )