Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 5, 2019

Kamati ya Bunge ya Miundombinu Yabaini kasoro Kadhaa kwa watumishi ATCL

juu
Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeitaka Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kusimamia ipasavyo nidhamu ya watumishi wake kwa sababu kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wateja kuhusu ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya watumishi wake.

Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni jana Jumatatu Februari 4, 2019, mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Kakoso alisema watumishi waajiriwe kwa kuzingatia vigezo vya sifa na uwezo.

Kakoso alisema changamoto zinazoikabili ATCL ni pamoja na uchache wa wataalam hususan marubani, nyenzo za kiutendaji hususan magari na madeni ambayo yameendelea kulingana na upatikanaji wa fedha.

Hata hivyo, Kakoso ameipongeza Serikali kwa jitihada za dhati na makusudi za kufufua kampuni hii ya ndege ya Tanzania kwa kununua ndege mpya sita.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )