Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 6, 2019

Kauli ya Serikali kuhusu Mauaji na Utekaji wa Watoto Mkoani Njombe

Serikali imesema si vyema kuhusisha mauaji ya watoto yaliyojitokeza mkoani Njombe na itikadi za aina yoyote au shughuli za uzalishaji mali na biashara kwani kwa kufanya hivyo inaweza kuwahusisha wasiohusika.
Hayo yamesemwa leo Jumatano Februari 6, 2019 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola wakati akitoa kauli za mawaziri.

Kauli hiyo ilikuja baada ya mbunge wa Lupembe (CCM), Joram Hongoli kuomba Bunge liahirishwe  Februari 4, 2019 ili wabunge waweze kujadili mauaji yanayoendelea mkoani Njombe.

Amesema watu 29 waliokamatwa ni wananchi wa kawaida usioweza kuwanasibisha na udini, siasa au biashara.

“Nashauri tutulie wakati Serikali kupitia wizara yangu tunaendelea kufuatilia na kudhibiti hali hii,” amesema.

Lugola amesema Serikali itawakamata wote waliosambaza taarifa za kuzua taharuki mitandaoni na kuwafikisha mahakamani ili wakajifunze kutumia uhuru wao wa kujieleza vizuri.

Pia amewaasa Watanzania kuacha kuanzisha na kusambaza taarifa za uzushi kwa nia yoyote  kwenye mitandao.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )