Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 16, 2019

Makonda Atoa milioni 5 ili kumsaidia kiuchumi mama yake Godzilla.

juu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Tsh. Milioni 5 kwa Mama mzazi wa Godzilla kama sehemu ya kutimiza malengo ya marehemu aliyokuwa ameyaweka kwa mama yake kabla ya kukutwa na umauti.

RC Makonda ameeleza hilo kwenye shughuli ya kuaga mwili wa mpendwa Godzilla inayofanyika katika viwanja vya Salasala Dar es Salaam.

"Ndugu yetu alikuwa na mipango wa kumsaidia mama yake kiuchumi, akawa amempa milioni nne lakini akawa na malengo ya kumpa milioni tano  ili aweze kuanzisha famasi kama sehemu ya kujitengemea kiuchumi," amesema.

Amesema kuwa baada ya Godzilla kuanza kuumwa mama yake alitumia fedha hizo, hivyo yeye atatoa Milioni tano ili kumuwesha mama Godzilla.

RC Makonda amesema fedha hiyo atatoa siku ya Jumatano na msanii Fid Q ndio atakabidhiwa ili akamkabidhi mama yake Godzilla.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )