Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 13, 2019

Mawaka ATCL Kuendelea Kusota Rumande

juu
Mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wanaokabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Sh10,874,280 kwa lengo la kuwakatia watu tiketi za ndege za shirika hilo wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi kutokakamilika.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 97 /2018 ni Fabian  Ishengoma (34), Adamu Kamara(27), Mlon  Masubo(29),  Alexander Malongo(24).

Wengine ni Tunu Kiluvya (32), Jobu Mkumbwa(30), Mohamed Issa (38), Godfrey Mgomela, Absalom Nyusi na Janeth Lubega(24).

Wakili wa Serikali, Janeth Magoa amedai leo Jumatano Februari 13, 2019  mbele ya hakimu mkazi mkuu, Salum Ally kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Wakili Magoa ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na hakimu Ally ameahirisha hadi Februari 26, 2019.

Washtakiwa wote wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la utakatishaji kutokuwa na dhamana.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )