Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 21, 2019

Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' Aachiwa kwa Dhamana

juu
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mhe. Joseph Mbilinyi 'Sugu' ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi jioni hii 

Mbunge huyo alishikiliwa tangu majira ya saa 1 asubuhi ya leo  Alhamisi tarehe 21 Februari, 2019  kwa tuhuma za kutoa/kutumia maneno ya uchochezi akiwa anazungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo. 

Kwamba vitambulisho vya wajasiliamali vimetolewa bila elimu na ni sawa na kunawa mikono kasha kwenda kujisaidia.

Kwa mujibu wa RPC Mbeya Urich Matei ni kwamba Mhe. Mbilinyi ameonekana katika moja ya clip ya video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akisikiliza hoja na malalamiko ya wananchi na kuyatolea ufafanuzi na ndipo alipoongea kwa kutoa msimamo wake kuhusu zoezi la ugawagi wa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogo ndogo @ wamachinga na kusema havifai vinastahili kuchomwa moto.

RPC Matei amesema Mhe.Mbilinyi alisikika akitumia maneno ya kashfa dhidi ya mamlaka iliyotoa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo ndogo pia kutumia lugha zinazopinga zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao.

Sugu ametakiwa kuripoti tena kesho asubuhi
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )