Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 9, 2019

Mfumuko wa bei wa taifa waendelea kushuka hadi asilimia 3.0

juu
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mfumuko  wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2019,umepungua hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2018.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii kutoka ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) Ephrahim Kwesigabo,wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini hapa.

Bw.Kwesigabo amesema kuwa hali hiyo inamanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma, kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2019 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2018.

Hata hivyo amesema Aidha  kuwa, kupungua kwa mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2019 kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za vyakula zikilinganishwa na zile zilizoishia mwezi Januari 2018.

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mweziJanuari 2019 umeendelea kupungua hadi asilimia 0.7 kutoka asilimia 1.0 ilivyokuwa mwezi Disemba 2018 “amesema Kwesigabo.

Aidha amezitaja  baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2019, ni pamoja na mchele kwa asilimia 3.9, mahindi kwa asilimia 13.9 na unga wa mahindi kwa asilimia 8.9.

Pia amesema kuwa bidhaa zingine ni mtama kwa asilimia 5.1, unga wa muhogo kwa asilimia 6.8, maharage kwa asilimia 4.2, chiroko kwa asilimia10.5, mihongo kwa asilimia 5.6, viazi vitamu kwa asilimia 3.3, magimbi kwa asilimia 18.6 na ndizi za kupika kwa asilimia 13.3.

Akizungumzia juu ya hali ya mfumuo wa bei kwa nchi za afrika mashariki amesema kuwa Nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Januari 2019 umepungua hadi asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.71 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2018.

“Kwa upande wa Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2019 umeongezeka hadi asilimia 2.7 kutoka 2.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2018 “amesema Kwesigabo
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )