Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 9, 2019

Muswada kupunguza mzigo wa kodi kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini wawasilishwa bungeni

juu
Serikali imewasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa 2 wa mwaka 2019 ambao unalenga kupunguza mzigo wa kodi  kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.

Muswada huo unapendekeza marekebisho katika Sheria ya Madini na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), uliwasilishwa leo Jumamosi Februari 9, 2019 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.

“Ili kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye madini ya metaliki na vito yatakayouzwa na wachimbaji wadogo wa madini kwenye masoko ya madini,”amesema.

Amesema lengo la mapendekezo hayo ni kuwahamasisha wachimbaji wadogo kuuza madini yao katika masoko ya madini na kudhibiti utoroshaji wa madini.

Profesa Kilangi amesema marekebisho hayo yanalenga kuweka ulazima wa ununuzi na uuzaji wa madini kufanywa katika masoko ya madini isipokuwa kwa wamiliki wa leseni kubwa na kati.

Amesema marekebisho hayo yanapendekeza vituo vya ununuzi wa madini vianzishwe katika maeneo ambayo hakuna masoko ya madini.

“Marekebisho hayo yanategemea kuweka mfumo madhubuti utakaowezesha wachimbaji wadogo kuuza madini yao,” amesema.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )