Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 5, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 66

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA      
 
Onyo langu likaeleweka, majira ya saa kumi na mbili alfariji Qeen na Latifa wakaondoka hotelini hapa na nikawahisi kwamba nitafika ofisini muda wowote. Nikajipumzisha hotelini hapa hadi majira ya saa sita mchana, nikajiandaa na kuanza safari ya kueleka ofisini kwangu tena kwa kutumia usafiri wa bajaji. 

Majira ya saa nen kasoro hikafika katika geti kuu na kuwakuta walinzi wa kampuni niliyo wapa dhamana ya kulinda ofisi yangu wakiwa wametanda katika geti hilo huku Biyanka akionekana kufoka sana na kuwaamrisha walinzi hao waweze kuondoka la sivyo atawafukuza kazi. 

Kutokana hakutarajia kuweza kuniona kwa wakati huu, taratibu nikashuka kwenye bajaji hii huku nikiishusha kofia yangu chini kidogo na kufika nusu uso. Watu wa pekee walio weza kunigundua na Qeen na Latifa ambao wapo mbele ya moja ya gari aina ya Costa wakisubiria kuelekea kwenye kampeni za mzee mkumbo.
   
ENDELEA   
Nikasimama karibu na geti hili,mlinzi mmoja akaniambia kwamba siruhusiwi kuingia kwa sasa na ofisi zimefungwa.
“Nisaidie kuniitia mkuu wenu”
Nilizungumza kwa sauti ya upole na ya chini kidogo, kutokana sifahamiki sana na walinzi, ikawa ni ngumu sana kwa mlinzi huyu kuweza kunitambua. Kiongozi akaja usawa wa eneo nilipo.
 
“Ni mimi fungua”
Mkuu wao akanifahamu, taratibu akawaamuru vijana wake kufungua geti dogo ambalo hutumika kupitia watu. Nikaingia ndani ya eneo hili huku nikivua kofia yangu na kuwafanya wafanyakazi wote katika eneo hili washangae hadi Biyanka mwenyewe akabaki akiwa na bumbuwazi.
“Watu wote murudi kwenye majukumu yenu ya kazi. Madereva rudisheni magari kwenye maeneo yake”
Baada ya kuzungumza hivyo wafanyakazi wakaanza kutawanyika.
 
“Ethan”
Biyanka aliniita huku akiwa katika hali ya upole na unyonge kwani lile ambalo amekusudia kulifanya limeshindikana na mbaya sikuweza kumueleza juu ya kuja kwangu nchini Tanzania.
“Twende ofisini”
Nilizungumza kwa msisitozo na kuelekea ndani, kila sehemu ninayo pita wafanyakazi wangu wananisalimia kwa furaha kubwa sana. Tukaingia kwenye lifti na taratibu ikatupeleka hadi gorofa ya juu kabisa, moja kwa moja nikaelekea ofisini kwnagu huku Biyanka akanifwata kwa nyuma.
 
“Oohoo jamani mume wangu ni suprize gani hii jamani!”
Biyanka alizungumza huku akijitahidi kujenga furaha usoni mwake. Kwajicho nililo mtazama ni ishara kwamba nimekasirika. Akataka kunikumbatia ila nikamzuia.
“Hivi ndivyo unavyo ongoza kampuni yangu?”
Nilizungumza kwa ukali na kumfanya Biyanka kukaa kimya kwa muda huku akinitazama usoni mwangu.
“Ndiyo unavyo ongoza kampuni yangu?”
“Ha…aaha.ahapana Ethan?”
“Ila, uhisi kila mmoja humu ndani ni mwanachama wa chama cha baba yako ehee?”
 
“Ethan umenifikiria vibaya?”
“Ujinga na upumbavu wako wote unao ufanya nimeuelewa na ninaufahamu. Usihisi kwamba nimekwenda kumzika mama yangu ndio sinto rudi nimerudi. Kama unahitaji kwenda kwenye mikutano ya kisiasa ya baba yako toka sasa hivi”
Nilifoka huku jasho likinimwagika usoni mwangu kwa hasira na kitu cha pekee ninacho jizuia kinywani mwangu ni kuropoka kwamba mimi ni mpizani wa baba yake na nipo kwa ajili ya kuiharibu familia ya baba yake.
Biyanka akakaa kimya huku akinitazama kwa wasiwasi mwingi sana.
 
“Hii ni kampuni yangu na hawa watu humu ni watu wangu. Mimi ndio mwenye maamuzi ya mwisho kwenye kila jamgo hivyo jitazame mara mbili Biyanka sitaki kampuni yangu ijihusishe na chama cha aina yoyote hapa Tanznaia. Itabaki kama kampuni ya kujitegemea kwa maana inatoa huduma kwa watu wa pende zote wawe chama tawala au wapinzani ila kinatoa huduma. Umenielewa?”
 
“Nimekuelewa”
“Nenda kwenye mkutano wa baba yako”
“Ethan mbona umekuwa ni mtu wa hasira sana?”
“Unanifanya niwe na hasira. Mama yangu amefariki, ni nani kati yenu ambaye ametoa japo hata pole ikiwa ni taarifa ambayo imesambaa kwenye mitando yote ya kijamii. Ehee au nyinyi hamkujua hilo?”
Biyanka akatazama chini akiashiria kwamba kile ninacho kizungumza ni kitu cha ukweli kabisa.
“Nimewajua nyinyi ni watu wa aina gani. Umenichukua niingie kwenye familia yako ili uweze kunitumia si ndio?”
“No no no no Ethan usingumze hivyo.”
 
“Ila unataka niendelee kuwakumbatia, kuwajali ikiwa nyinyi hata pole hamjafanya. Una account ya Twitter, Instergram na Facebook. Ila hakuna hata sehemu uliyo andika pole. Huku ukidai kwamba wewe ni mke wangu, mwanamke wa maisha yangu. KIVIPI……..EHEEEE?”
“Ethan akili zetu tumechanganyikiwa, kampeni zinatuendea mrama. Watu wamekuwa ni wasaliti, hawaonekani kabisa kwenye mikutano ya baba yangu. Nakuomba sana mpenzi wangu unisamehe. Tambua mkeo na familia yangu kwa ujumla tupo kwenye mapambano makubwa sana. Ninakuomba sana Ethan unielewe”
 
“Okay nenda kwenye kampeni. Tutazungumza baadae”
“Ethan!!!”
“Elewa kitu ninacho kizungumza Biyanka alaa!! Nahitaji kuwa peke yangu sasa”
Biyanka akanitazama kwa macho ya upole kisha akageuka na kutoka ndani humu, akaubamiza mlango wa ofisi yangu kwa nguvu na kunifanya niachie msunyo mkali sana. Nikanyanyua simu yangu ya mezani na kumpigia sekretari wangu, baada ya muda kidogo akaingia.
 
“Ndio mkuu”
“Itisha kikao cha wafanyakazi wote kwenye ukumbi wa mikutano gorofa ya tano”
“Sawa mkuu”
Sekretari akaondoka na kuniacha peke yangu. Mawazo mengi sana juu ya kuhakikisha kwamba ninawapokonya kila kitu wanacho kihitaji hii familia ya bwana Mkumbo, bado yanaendelea kunijaa kichwani mwangu, huku kila ninacho kipanga ninakiona hakiki sawa. Nikapata wazo moja kubwa sana ambalo kwa namna moja limtamchafua bwana mkumbo yeye na chama chake.
 
“Mkuu kikao tayari”
Sauti ya sekretari wangu ikanitoa kwenye dibwi hili la mawazo. Nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kalia na kuongozana naye. Tukaingia kwenye ukumbi huu mkubwa ulio jaa wafanyakazi wote wa kampuni yagu. Nikasimama kwenye jukwaa na kuwatazama wafanyakazi wote kwa muda wa kama dakika tano, kisha taratibu nikashusha pumzi.
 
“Habari yenu”
“Salama mkurugenzi”
Nikasogeza karibu kipaza sauti na kuendelea kuzungumza.
“Kwajambo lililo jitokeza leo. Sinto hitaji lijitokeze tena kwenye kampuni hii pasipo idhini yangu mimi. Kapuni yangu si kampuni ya siasa, wala si kampuni ya kumpigia kura mtu gani. Hata ikitokea mimi nina gombea uraisi, sito mlazimisha hata mmoja wenu  aje kwenye kampeni zangu eti kisa mimi ni mkurugenzi wako. Hapana hicho kitu hakita jitokeza”
Nikanyamaza kidogo huku nikisikilizia makofi yanayo pigwa na wafanyakazi wangu ambao wnaaonekana kururahishwa na hichi nilicho kizungumza.
 
“Nimepitia account zenu kipindi nipo nyumbani nchini Ujerumani.  Asanteni kwa kunipa pole kwa kile ambacho kimetokea kwenye familia yangu. Nina imani kwamba wengi wenu mulishangaa kwa kuondoka kwangu gafla pasipo taarifa yoyote kwenu. Nimerudi na nitaongoza kampuni yangu katika mstari ambao siku zote huwa ninauamini. Upendo, uchapakazi na hekima. Ndio vitu vinavyo niongoza toka nilipo kuwa mtoto mdogo”
 
“Kama kuna malalamiko yoyote ambayo yametokea kwa kipindi hichi cha wiki tatu ambazo sikuwepo hapa nchini. Ninawaomba muweze kuniandikia malalamiko hayo kwa siri sana, kisha mutamkabidhi sekretari wangu na atayawasilisha ofisini kwangu. Naweka siri kwa manaa wengi wenu natambua kwamba muna muogopa meneja Biyanka. Hivyo fanyeni katika utaratibu nilio waagiza sawa”
“Sawa”
 
Mfanyakazi mmoja akanyoosha mkono juu, nikamruhusu aweze kuzungumza.
“Kwanza kwa niaba ya wafanyakazi wote. Tunapenda kukupa pole kwa mara nyingine mkurugenzi, tulitamani kutuma japo wawakilishi wawili kwenye msiba ila kwa jibu alilo tupa meneja nina imani kwamba kila mmoja wetu hapa ana lifahamu”
“Jibu gani lizungumze usilifumbe fumbe?”
“Ahaa si jibu la kiungwana mkurugenzi ni jibu ambalo linaweza kupelekea mtafaruku kidogo kwenye mahusiano yenu”
“Wewe kuwa na amani, zungumza ni jibu gani?”
“Ngoja nimsaidie muheshimiwa”
“Sawa mama zungumza”
 
“Meneja alisema kwamba yeye ndio mwana familia wako hivyo msiba hautuhusu wawakilishi watulize mishono yao na waendelee na majukumu ya kazi kama kawaida”
“Mishono ndio nini?”
“Kwa lugha nyepesi mkuu niseme ni kihere here”
“Nashukuru sana mama yangu. Endelea kaka”
“Ndio hivyo muheshimiwa, tulishindwa na tukaona tuji organize kimya kimya. Tukachanga kijimchango kidogo naona mtuza pesa wetu tuliye mchagua hapo anaweza kuzungumza”
 
“Nani mtunza pesa?”
Akasimama msichana mmoja mpole kwa kumtazama.
“Ndio zungumza”
“Tumeweza kukusanya kiasi cha shilingi milioni kumi na tano mkuu na pesa yote hiyo ipo benki”
“Nawashukuru sana. Zawadi muliyo nipatia hakika ni kubwa sana kwangu ninawashukuru sana”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu kwani sikutarajia kama wafanyakazi wangu wana umoja kiasi hichi na hii ni ishara moja nzuri inayo onyesha kwamba hata siku  nikipata tatizo basi wanaweza kuungana kwa pamoja na kunisaidia.
 
“Mama yangu alifariki kwa saratani pia kwa baba ndio hivyo hivyo. Pesa iliyo patikana nitaongezea na kiasi kingine na kwa pamamoja tunatembelea hospitali inayo shuhulika na magonjwa hayo na kutoa kiasi hicho ili wagonjwa waendelee kufanyiwa matibabu na kama Mungu anaweza kuwajalia basi waweze kupona”
Nilizungumza kwa upole na wazo langu likaonekana kupokelewa na wafanyakazi wangu wote.
“Nawashukuru kwa muda wenu na moyo wenu wa kujitoa na Mungu awabariki”
“Nawe pia mkurugenzi”
Nikatoka ukumbini humu na kuacha minong’ono mingi kwa wafanyakazi. Nikarudi ofisini kwangu, nikapokea ujumbe wa simu kutoka kwa Qeen akinitaarifu kwamba Roman amesha kamilisha kazi niliyo mkabidi.
‘YUPO WAPI’
Nilimjibu kwa ujumbe mfupi wa meseji.
‘KAMA HUTO JALI TUKUPELEKE’
‘SAWA BAADAE TUTAKWENDA’
‘SAWA MKUU’
Nikafuta meseji zote. Baada ya muda sekretari akaingia akiwa ameshika karatasi nyingi.
“Yote hayo ni maoni?”
“Ndio mkuu”
 
“Mmmmmm kazi kweli kweli. Inaonekana kuna madudu yalitokea mengi sana kipindi mimi sipo?”
“Yapo mengi ila ndio  hivyo mkuu wetu alikuwa anafanya vile anavyo jisikia yeye.”
“Hembu niambie kwa ufupi, alikuwa anafanya nini?”
“Ukiachilia na swala hili la leo la kulazimiswa kuelekea kwenye mikutano wa baba yake. Mwezi ulio isha juzi, kila mtu amekatwa elfu hamsini hamsini kwenye mshahara wake, kilazima ili kuweza kuchangia kampeni za baba yake”
“Fu** Huyu mwanamke anahitaji nini kwangu.?”
 
Nilizungumza kwa jazba kidogo kwa maana upuuzi alio ufanya Biyanka ni wa kushangaza kwa kwlei.
“Jambo jengine, kuna wafanyakazi kumi wamefutwa kazi”
“Wamefutwa kazi kwa kosa gani?”
“Walikuta wakijadili maswala ya chama pinzani kwenye group la whatsapp ambalo tumejiunga wafanyakazi wote. Ila Meneja mkuu hayupo kwenye hilo group ila kuna vibaraka wake wamempelekea ushahidi wa wafanyakazi hao jinsi walivyo kuwa wakimuunga mkono mpinzani wa baba yake. Na ndio hivyo wamefukuzwa kazi”
“Hao walio fukuzwa kazi ni nani na nani?”
“Kwamajina kwa haraka haraka siwafahamu. Ila wapo kwenye takwimu zangu ofisini”
 
“Sasa wapigie simu wote. Waambie mkurugenzi kesho asubuhi, saa mbili ana wahitaji warudi kazini nakabla ya hawajaanza kazi wakutane na mimi tuzungumze kwanza. Sawa?”
“Sawa mkuu”
“Unaweza kuendelea na majukumu yako”
Sekretari wangu alipo toka, nikaanza kupitia maoni ya wafanyakazi wangu na wengi wanalalamika kwa swala la wao kukatwa mishahara. Nikampigia muhasibu wa kampuni na kumuita ofisini kwangu.
“Karibu ukae Mr Merema”
“Nashukuru mkuu”
“Mauzo kwa wiki tatu yamepanda au yameshuka?”
“Yameongezeka kwa asilimia mbili mkuu. Tofauti na uwepo wako kazini”
 
“Sawa, kuna swala nimelisikia la watu kukatwa elfu hamsini hamsini kwenye mishahara yao hilo limekaaje?”
“Ni kweli, mimi nililetewa oda na meneja mkuu nami sikuwa na pingamizi na nikafanya kama alivyo niamrisha japo nilijaribu kumshauri ajaribu kuzungumza na wafanyakazi ila ila akakataa na kunipa vitisho vya kunifukuza kazi muhesimiwa”
“Sasa kila mfanyakazi arudisiwe pesa yake leo hii na ujinga huo sihitaji ujitokeze tena kwenye kampuni hii. Nimekupa dhamana ya pesa zangu simamia. Mtu anaye weza kukufukuza kazi ni mimi. Umenielewa?”
“Nimekuelewa mkuu”
“Nashukuru”
 
Muhasibu akanyanyuka na kuondoka eneo hilo la hapa ofisini. Muda wa kutoka ofisini ulipo wadia, nikaondoka ofisini hapa huku nikikodi bajaji kurudi hotelini nilipo fikia. Majira ya saa nne usiku Roman akaja kunichukua hotelini hapa na moja kwa moja akanipeleka hadi katika godauni moja lililopo katika mji wa Bagamoyo. 

Tukaingia kwenye godauni hili lenye ukimya huku kofia yangu nyeusi nikiwa naimeivaa vizuri kichwani mwangu na kuficha kabisa sura yangu. Kwa mavazi haya meusi niliyo yavaa si rahisi kwa mtu kuweza kunitambua kwamba ni mimi. 

Tukaingia katika chumba ambacho amemning’iniza mzee huyu kichwa chini miguu juu huku akiwa amemvua nguo zote na kumbakisha na boksa tu na usoni mwake amemfunga kitambaa cheusi ambacho si rahisi kwa mzee huyu kuweza kuniona. Nikamtazama mzee huyu na wazo la kuweza kumchafua mzee Poul Mkumbo taratibu likaanza kunijaa kichwani mwangu na nikaona muda huu ndio mzuri wa kuweza kutekeleza kile nilicho kikusudia kukifanya.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )