Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imezitaka halmashauri kote nchini kuwa na mpango mkakati wa kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya bajeti ya ujenzi wa mabweni ya watoto wa kike ili kupunguza tatizo la Mimba kwa watoto wa kike hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo Februari 8 bungeni Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mwita Waitara wakati akijibu Swali la mbunge wa jimbo la Rombo [CHADEMA] Joseph Selasini aliyetaka kujua kwanini serikali isiagize halmashauri kujenga mabweni kwa lazima na si hiari ili kuepusha watoto wa kike kupata mimba na kukatiza ndoto zao.
"Mimba za watoto mashuleni ni jambo la aibu kwelikweli na sisi kama wazazi lazima tulichukulie very serious .Kama tulivyoanza program ya kujenga madarasa shule za kata ,kwanini serikali isiagize yajengwe mabweni na si kwa hiari kwa sababu hawa watoto wanapata mimba kutokana na njaa hawa bodaboda"
Akijibu swali hilo ,Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amesema jambo la kujenga mabweni hususan ya watoto wa kike ni la lazima hivyo amezitaka halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya mabweni hasa katika mwaka huu wa uandaaji wa bajeti za halmashauri.
Bunge la 11 mkutano wa 14 kikao cha 10 hati mbili zimewasilishwa ambazo ni hati ya fedha No.1kwa nusu ya kwanza 2018/2019, na ile ya uhamilishaji fedha No.2 nusu ya kwanza 2018/2019 na tamko la mapitio ya fedha nusu ya kwanza 2018/2019 huku jumla ya maswali 14 yakiulizwa na kujibiwa na wizara husika.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )