Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 12, 2019

Urusi yajipanga kuzima Intaneti ili kujilinda na maadui

juu
Urusi inajipanga kuzima mtandao wa intaneti kwa muda, na hivyo kujitoa kwenye mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao.

Zoezi hilo litafanya mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala  ya kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.

Rasimu ya sheria ya kuruhusu mabadiliko ya kiufundi ili kuiwezesha nchi hiyo kuendesha mtandao wake wenyewe iliwasilishwa bungeni mwaka jana.

Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe mosi Aprili, lakini siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijatajwa.

Rasimu hiyo ya sheria, iliyopewa jina la Programu ya Taifa ya Uchumi wa Kidijiti, inawataka watoa huduma za intaneti nchini Urusi kuwa na uwezo wa kuendelea na huduma zao hata pale ikitokea nchi za kigeni zikiamua kuitenga Urusi.

Nchi wanachama wa Nato na washirika wake wamekuwa wakitishia kuiwekea vikwazo vya kimtandao Urusi ambayo wanaituhumu kwa kufanya mashambulio ya kimtandao.

Njia mojawapo inayopangwa na Urusi katika kujilinda huko ni kutengeneza mfumo wake binafsi wa anuani za kimtandao ufahamikao kama DNS, waweze kupata mawasiliano hata pale watakapotengwa ama kujitenga.

Kwa sasa, kuna taasisi 12 zinzoshughulikia suala la utolewaj na matumizi ya anuani hizo na hakuna hata moja iliyopo Urusi.

Hata hivyo tayari kuna chapa nyingi za mfumo huo wa DNS nchini Urusi hali inayoonesha kuwa nchi hiyo inaweza kuendelea na shughuli zake za kimtandao hata ikitokea imetengwa leo.

Watoa huduma za intaneti wanatarajiwa kuelekeza mawasiliano yote yanayopita kwao kwenye vituo vya serikali kwenye zoezi hilo. Mawasiliano yote ya ndani ya Urusi yataruhusiwa kuendelea lakini yale yatokayo nje ya nci yataminywa.

Mwishowe, serikali ya Urusi itakuwa na ubavu kama wa China wa kupanga mawasiliano gani raia wake wapate kutoka nje ya nchi. 

Credit:BBC
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )