Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, March 16, 2019

Auawa Wakati Akijaribu Kupora Pikipiki

juu
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
OMARY Abdallah maarufu Mboweto (50) mkazi wa Kagera ,Dar es salaam aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi ,kijiji cha Malale kata ya Vihingo, Mzenga Kisarawe mkoani Pwani,baada ya marehemu akiwa na washirika wenzake wawili kufanya jaribio la kupora pikipiki huko Maneromango.
 
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema, tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia march 15 mwaka huu.
 
Alieleza, marehemu kabla ya kuuawa akiwa na wenzake wawili wakitumia gari namba T. 613 DFG aina ya carrina walifika Maneromango na kufanya tukio hilo.
 
“Baada ya wananchi kuwashtukia ndipo marehemu alikimbiza gari kwa lengo la kukimbia.
 
“Walipofika katika cha Vihingo, gari lao lilipata ajali ya kuingia kwenye korongo ambapo waliacha gari hilo na kukimbia ndipo wananchi waliwakimbiza na kumshambulia marehemu kwa silaha mbalimbali za jadi na mawe na kusababisha kupoteza maisha “alifafanua Wankyo.
 
Wankyo alieleza, mtuhumiwa mwingine mmoja Abdul Zuberi maarufu Mvidunda (35)mkazi wa Chamazi alikamatwa maeneo ya Sumbwi wakati akijaribu kutoroka.
 
Watuhumiwa baada ya kuhojiwa wamekiri kujihusisha na matukio mawili ya uporaji tarehe 14 January mwaka huu huko Kitonga Kisarawe ambapo walipora pikipiki aina ya sanlg namba MC 324 CDL aina ya haoujue mali ya Haruna Goha.
 
Wankyo alisema, tukio jingine walilolifanya ni kupora bajaji eneo la Kibuta mali ya Shukuru Ally february 13 mwaka huu.
 
Aidha jeshi la polisi mkoani hapo, limewakamata Ally Said maarufu kwa jina la Sober (37)Ramadhani Hamza -Mijoke (40)na Said Ramadhani -Ubwabwa (37)wakazi wa Mwendapole wakijihusisha na uhalifu wa kushusha mizigo katika magari,yanayotumia barabara kuu ya Dar es salaam kwenda Morogoro kwa jina maarufu Lumbesa /Shushashusha.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )