Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, March 3, 2019

Jaji Mkuu aagiza kupelekewa mashauri ya mirathi nchi nzima

juu
Lydia Churi-Mahakama, Mtwara
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameagiza kupelekewa mashauri yote ya Mirathi nchi nzima ili aweze kujua ni changamoto gani inayofanya yachelewe kumalizika na kupanga mkakati wa kisheria ili mashauri hayo yawe yanaisha ndani ya muda uliowekwa kisheria.

Akizungumza katika ziara yake ya kikazi aliyoanza jana mkoani Mtwara, Jaji Mkuu alisema katika mahakama za Mwanzo mashauri hayo yanatakiwa uisha ndani ya miezi sita lakini yapo mengine yamekaa zaidi ya miaka kumi.

Alisema kutokana na kuchelewa kumalizika kwa mashauri haya, wakati mwingine humfanya msimamizi wa mirathi kuendelea kunufaika na mali za marehemu wakati warithi wapo na wanataabika kwa muda mrefu.

Jaji Mkuu amesema ametoa agizo hilo pia kwa kuwa mashauri ya aina hiyo huweza kuzalisha migogoro mingi katika jamii na kusababisha haki kutokupatikana kwa wakati.

Akizungumzia changamoto nyingine zinazoikabili Mahakama ya Tanzania katika kutekeleza jukumu lake la msingi la utoaji wa haki, Prof. Juma alisema Mahakama inakabiliwa na changamoto kubwa ya wananchi kutofahamu taratibu za kisheria jambo linalosababisha washindwe kupata haki kwa wakati.

Alisema hivi sasa Mahakama ya Tanzania imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya taratibu za kisheria kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Mahakamani ili kuwasaidia wanannchi kutambua nini cha kufanya

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama imeamua kuwa wazi katika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni moja ya hatua muhimu za mapambano dhidi ya rushwa ndani ya Mhimili huo.

Awali akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, Jaji Mkuu aliwaomba wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini kushirikiana na Mahakama ya Tanzania katika kuwaelimisha wananchi taratibu za mchakato wa upatikanaji wa haki.  

Alisema Mahakama inachangia utulivu na Amani katika nchi pale inapotekeleza jukumu lake la msingi la utoaji wa haki kwa wakati na endepo Mahakama haitafanya kazi yake vizuri ni wazi itatoweka. Aliongeza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 pia imetoa mwelekeo wa Amani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akimkaribisha Jaji Mkuu Ofisini kwake alisema Serikali kupitia Mkoa wake inashirikiana vizuri na Mahakama katika kuwahudumia wananchi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.

Wakati huo huo, Mtendaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Bwn. Solanus Nyimbi alisema  ili kutatua changamoto ya uchakavu na ukosefu wa miundombinu ya Mahakama hususan majengo, Mhimili huo umeandaa Mpango Kabambe wa ujenzi uliozingatia maeneo yanayotakiwa kujengwa majengo mapya ya Mahakama, pamoja na yanayotakiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Alisema hivi sasa majengo yanayoendelea kujengwa ni pamoja na Mahakama za Mwanzo 22, Mahakama za Wilaya 20, Mahakama za Mikoa (Hakimu Mkazi) 8 pamoja na Mahakama kuu 2, zinazojengwa katika mikoa ya Mara na Kigoma.

Alisema wilaya ya Tandahimba nayo iko kwenye mpango wa kupatiwa jengo litakalojumuisha mahakama ya Wilaya pamoja na Mahakama moja ya Mwanzo. Aliongeza kuwa lengo ni kuwa na Mahakama katika kila makao makuu ya Tarafa.

Bwn. Nyimbi alisema ifikapo mwaka 2021 wilaya zote zisizo na majengo ya Mahakama zitakuwa tayari zimepatiwa majengo hayo ambapo ujenzi huo utatumia fedda za ndani pamoja na za Benki ya Dunia.

Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi aliyoianza leo katika mkoa wa Mtwara. Alitembelea Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara pamoja na Mahakama ya wilaya ya Tandahimba ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )