Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 14, 2019

Upelelezi Kesi ya Wanaodaiwa kughushi saini ya waziri Makamba wakaribia Kukamilika

juu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili wafanyakazi watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) unakaribia kufikia mwisho.

Kesi hiyo ilipangwa jana kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Janeth Mtega.

Wakili wa Serikali, Jenipher Massue, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi unakaribia kufikia mwisho na maendeleo ya kesi hiyo ni mazuri.

"Mheshimiwa Hakimu kesi hii upelelezi wake unakaribia kufika mwisho na maendeleo ni mazuri. Tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa ili kuja kuangalia kama tutakuwa tumekamilisha kipengele kilichobakia," alidai Wakili Massue.

Wakili wa Utetezi, Bernard Mbakileki, aliwaomba mawakili wa serikali siku ya tarehe nyingine ya kesi hiyo waje na taarifa nzuri zaidi ili kila upande ujue hatima yake katika kesi hiyo.

Hakimu Mtega alisema kesi hiyo itatajwa Machi 27, mwaka huu, na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Wafanyakazi hao wanakabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa mazingira na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, hivyo na kusababisha hasara ya Sh. milioni 160.

Washtakiwa hao ni Ofisa wa Mazingira NEMC, Deusdedit Katwale (38) na Mtaalamu wa IT, Luciana Lawi (33) wote wakazi wa Ubungo Msewe, Katibu Muhtasi wa NEMC, Edna Lutanjuka (51) Mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, Msaidizi wa Ofisi Mwaruka Mwaruka (42) na Ofisa Mazingira wa NEMC, Lilian Laizer (27), wote wakazi wa Ukonga Mombasa na Ofisa Mazingira wa NEMC, Magori Wambura (38) mkazi wa Bombambili.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Septemba 27, 2016 na Aprili Mosi, mwaka jana, jijini Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )