Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, April 24, 2019

Diamond Ataja Sababu za Kuacha Kuwahudumia Watoto Wake Aliozaa na Zari

juu
Msanii Diamond Platnumz ameeleza kile kinachoendelea kati yake na mzazi mwenzie Zari The Bosslady kuhusu watoto wao.

Muimbaji huyo kwenye kipindi cha Block 89 kupitia Wasafi FM amesema Zari amekuwa akizuia pindi anataka kuwaona watoto wake.

Amesema kila mwezi alikuwa akitoa dola za Marekani 2,000 ambazo ni wastani wa Sh5 milioni kwa ajili ya matunzo ya watoto. 

“Niseme ukweli kabisa, nina kama miezi mitatu hivi sijapeleka fedha za matunzo ya watoto kwa sababu mwenzangu hataki hata niongee na watoto, hebu fikiria hata kupitia mfanyakazi wa ndani amegoma nisiongee nao.

“Nilijaribu kuwasiliana na mtoto wake wa kiume, yule mkubwa  lakini mwenzangu ameniwekea ngumu,” amesema.

Jitihada nyingine anazosema mwenzake amekuwa akizizima ni za kuwaleta watoto nchini akisema amemuwekea masharti kuwa lazima aje nao.

“Zari anataka aje na watoto, mimi nimemwambia mama nina mahusiano mengine nikamshauri mama yangu mzazi awafuate watoto lakini akakataa akasema labda niende kuwaangalia Sauzi (Afrika Kusini),” amesema.


Ameendelea kueleza kuwa, "Kuna kipindi Tiffah alizidisha muda wa kukaa South kwasababu anapassport ya Tanzania, ningekuwa nataka matatizo ningeweza kupiga simu mtoto akarudishwa Tanzania".
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )