Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 12, 2019

Kesi ya Kigogo TAKUKURU Yapigwa Kalenda

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa mipango, ufuatiliaji na tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor umeiambia Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la utakatishaji wa fedha kiasi cha zaidi ya Sh 1.477 bilioni.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo leo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mshtakiwa huyo  alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Machi 29 hivyo leo ni mara ya pili kesi hiyo imetajwa na kwamba bado wananaendelea na upelelezi.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 25 na mshtakiwa amerudishwa rumande.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )