Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, April 15, 2019

Mkuu wa Mkoa, Wilaya atakae msweka mtu mahabusu bila sababu kuchukuliwa hatua

juu
Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wenye tabia ya kuwasweka mahabusu watu wasiokuwa na hatia watachukuliwa hatua.

Mkuchika amesema kuwa mtu anawekwa ndani kama ana hatarisha amani sio watu wanadaiana madeni huko una muweka ndani, mtu asiwekwe mpaka awe amehatarisha amani.

“Hao wakuu wa Mikoa na Wilaya hawatatetewa na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ninamshukuru mwanasheria mkuu wa Serikali ametoa waraka kwa wote waliopewa mamlaka ya kuweka mtu ndani na mimi kanipa nakala, ikieleza mazingira ya mtu kuwekwa ndani,” amesema Mkuchika lleo Jumatatu Aprili 15, 2019 bungeni jijini Dodoma na kuongeza;
 

“Huyo mtu ni lazima kwanza  awe ametenda kosa la jinai, na (mkuu wa wilaya, mkoa) uweke kwa maandishi kwa nini umemuweka ndani. Utawala bora unasema kesi ikiwa mahakamani hakuna mkuu wa wilaya, mkoa au waziri anayeweza kuisikiliza.”

Mkuchika amesema wakuu wa wilaya na mikoa wanapotumia mamlaka yao kuweka mtu mahabusu kwa saa 24 na 48 wazingatie sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997.

“Sheria hii inawapa mamlaka kuwaweka ndani watu pale inapothibitika anahatarisha amani. Nawaomba wabunge tusikilize sheria na nawaomba na huko walipo (wakuu wa wilaya na mikoa) wanisikilize,” amesema.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )