Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, August 12, 2019

Boti Yapinduka Bahari ya Hindi Ikiwa na Watu 11

juu

Boti inayomilikiwa na klabu ya starehe ya Yacht jijini Tanga, imepinduka baharini jana jioni Agosti 11, 2019, ikiwa na watu 11 wengi wao wakiwa ni wafanyakazi wa Benki ya NMB Korogwe.
 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Edward Bukombe, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

 “Baada ya watu hao kupanda boti hiyo, ambao walikuwa wakienda kutembelea visiwa mbalimbali vilivyopo kwenye bahari hiyo na ndipo upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi walipotoka ndipo ilipopinduka na kuwamwaga.

“Kwenye boti hiyo kulikuwa na watu 11 ambapo 10 kati yao waliokolewa kutokana na kuvaa maboya wakati wakiwa baharini na mwingine mmoja ambaye inadaiwa hakuwa nayo hadi sasa hajulikani alipo,” amesema.

Aidha, Kamanda Bukombe ametoa wito kwa wananchi wanaotumia bahari kusafiria kuchukua tahadhari wanapokuwa baharini kwa kuhakikisha wanavaa maboya ya kujiokolea ili wakati yanapotokea majanga kama hayo waweze kuona namna ya kujiokoa.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )