Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, September 20, 2019

Mahakama Kuu Yaamuru Fatma Karume asiendelee kuwa Wakili

juu
Mahakama Kuu imeamuru Wakili Fatma Karume asiendelee kuwa Wakili kwa muda kutokana na upande wa Serikali kulalamikia matamshi yaliyotolewa na Wakili huyo katika kesi iliyofunguliwa na Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Ado shaibu dhidi ya Rais John Magufuli na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Karume amesimamishwa leo Ijumaa Septemba 20, 2019 huku sababu ikitajwa kuwa ni alichokizungumza katika kesi iliyofunguliwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Adelardus Kilangi aliyeteuliwa na  Rais John Magufuli Februari Mosi, 2018.

Shaibu amesema mawakili wa Serikali walilalamikia maneno yaliyoandikwa na Fatma wakati wanafungua kesi hiyo Mahakama Kuu.

“Maneno yenyewe aliyoyatumia ni commitment yake ya kwamba ‘hata kama kesi hii itashindwa ataendelea kupambana nayo, Rais akiondoka madarakani mwaka 2020 au kama ataondoka 2025 au kama mahakama itabadilika ataendelea kupambana’.”

“Na kwamba upande wa mwanasheria mkuu wanamtetea Rais Magufuli kwa hiyo wanasema ni kama amewa-attack, amemu-attack Mwanasheria Mkuu, hivyo wakasema inabidi apelekwe kwenye kamati ya maadili ya mawakili na wakati suala lake likijadiliwa atakuwa amesimamishwa uwakili,” amesema Shaibu.

Shaibu amesema uamuzi huo umetangazwa leo huku madai katika kesi ya msingi yakitupiliwa mbali kwa hoja kwamba Rais hawezi kusimamishwa mahakamani.
 
Alipoulizwa kuhusu hatua hiyo dhidi yake, Fatma amesema anakusudia kufungua kesi Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) kupinga kusimamishwa kwake uwakili bila kupewa nafasi ya kujieleza.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )