Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, September 21, 2019

Marekani kupeleka vikosi zaidi vya kijeshi nchini Saudi Arabia baada ya shambulizi dhidi ya kiwanda cha mafuta

adv1
Rais Donald Trump ameidhinisha hatua ya kupeleka vikosi zaidi vya kijeshi Saudi Arabia kusaidia vikosi vya ulinzi vya angani nchini humo. Hii ni baada ya shambulizi lililoharibu viwanda vikuu vya mafuta nchini humo.
 
Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper amethibitisha hatua hiyo ya kupelekwa kwa vikosi hivyo zaidi vya kijeshi nchini Saudi Arabia jana Ijumaa. 

Idadi kamili ya maafisa wa kijeshi na vifaa vitakavyotumiwa bado haijabainika lakini itakuwa sehemu ya "uhamishaji wa wastani'' katika eneo hilo. 

Hii ni kulingana na jenerali wa jeshi la wanamaji Joseph Dunford, ambaye ni mwenyekiti wa kundi shirikishi la wakuu wa kijeshi.

"Kwa kujibu ombi la taifa hilo la kifalme, rais ameidhinisha kupelekwa kwa vikosi vya kijeshi vya Marekani ambavyo vitatekeleza jukumu la ulinzi  na kuangazia zaidi ulinzi wa angani na makombora," Esper aliwaambia wanahabari.

Tangazo hilo linajiri baada ya shambulizi la Sepetmba 14 dhidi ya muundo msingi mkuu wa mafuta nchini Saudi Arabia ambalo lilitatiza nusu ya usambazaji wa bidhaa ya mafuta nchini humo. 

Waasi wa kihouthi nchini Yemen wamedai kuhusika katika shambulizi hilo lakini Marekani na Saudi Arabia zinashuku kuwa Iran ndio iliyohusika. Iran inayoungwa mkono na kundi hilo la kihouthi, imekanusha madai hayo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )