Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, September 2, 2019

Watu zaidi ya 100 wauliwa Yemen na ndege za Suadi Arabia

juu
Yemen bado imo katika mshtuko baada ya watu zaidi ya 100 kuuliwa kutokana na mashambulio yaliyofanywa na ndege za muungano unaoongozwa na Saudi Arabia. 

Mashambulio yaliyokuwa mabaya kabisa mnamo mwaka huu yalifanyika kwenye kituo cha mahabusu kinachosimamiwa na waasi wa Kihouthi. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa katika hujuma hiyo ya majeshi ya nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia. 

Mahabusu wapatao 170 walikuwamo kwenye kituo hicho kilichopo kwenye jimbo la Dhamar la kusini magharibi mwa Yemen. 

Shirika la misaada la Msalaba Mwekundu limesema watu 40 waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu lakini wengine wanahofiwa kuwa wamekufa. 

Mkuu wa shirika hilo nchini Yemen amesema idadi ya waliokufa inaweza kuwa kubwa zaidi. Nchi zilizofungamana kijeshi na Saudi Arabia katika vita vya nchini Yemen zimeshutumiwa vikali duniani kwa kufanya msahambulio ya ndege ambayo mara nyingine yamezilenga shule, hospitali na pia sherehe za harusi na kusababisha vifo vya maelfu ya raia. 

Tangu mwaka 2015, Mfungamano wa nchi hizo umekuwa unapambana na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )