Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, September 16, 2019

Wizara Ya Kilimo Yafanya Maaandalizi Ya Sera Mpya Ya Kilimo

juu
Waziri wa Kilimo Japheti Hassunga leo  amekutana na Menejimenti ya wizara,wakuu wa Taasisi na  Wenyeviti wa Bodi za Mazao  zilizopo chini  ya Wizara.  

Lengo la mkutano huu wa siku mbili unaofanyika  katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma  ni kujadili maandalizi ya sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019 na kuondoa mapungufu yaliopo katika sera ya mwaka 2013. 

Akiongea katika kikao kazi hicho Waziri  Hasunga ameeleza umuhimu wa kuwa na sera mpya ya kilimo ni kufanya kilimo kuwa na tija na cha kibiashara ,hivyo kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo 

“Tunataka sera mpya ya kilimo ilenge kukifanya kilimo kuwa shughuli kuu ya kiuchumi itakayochangia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira” alisisitiza Waziri Hasunga. 

 Waziri Hasunga amebainisha kwamba sera mpya  inatakiwa kukamilika  kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kutoa fursa kwa Bunge kutunga sheria na kanuni za kilimo. 

Aidha katika mkutano huu wizara ya kilimo itajadili na kupitia taarifa ya utekelezaji wa shughuli kwa mwaka 2018/2019 na kuweka mkakati madhubuti wa utekelezaji mipango utendaji kazi ya wizara kwa mwaka 2019/2020. 

Kikao hicho kinahudhuriwa na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba,Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu Prof.Siza Tumbo. 

Mwisho.
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo-DODOMA
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )