Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, November 26, 2019

Taarifa Ya Jeshi la Polisi Kwa Umma toka Mkoa wa Mbeya

adv1
 JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 11 kwa tuhuma za kupatikana na Pombe Moshi na Bhangi katika misako na doria zilizofanyika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo:-

KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko Mtaa wa Majengo mapya tazara, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Askari Polisi walimkamata PASCHAL ULEDI [31] kondakta wa daladala na mkazi wa Iwambi akiwa amepanda miche nane [8] ya bhangi nyumbani anapoishi. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO]
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko maeneo ya Mtaa wa Kagera, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata ROIDA IJANDE [60] mkazi wa Mama John akiwa na pombe haramu ya moshi lita ishirini [20]. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 saa 14:40 mchana huko Mtaa wa Mwatengule kwenye kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo Kata ya Isyesye, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata JANEPHA COSMAS [28] mkazi wa Isyesye akiwa na pombe haramu ya moshi kiasi cha lita moja na nusu ikiwa kwenye chupa ndogo ndogo 15 pamoja na bhangi uzito wa gram 280. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe haramu @ gongo na bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 15:00 alasiri huko maeneo ya Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata ENNY [65], mkazi wa Airport akiwa na pombe haramu ya moshi lita 5 kwenye kidumu cha lita tano. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 15:05alasiri hadi saa 17:00 jioni umefanyika msako maeneo mbalimbali ya Kata za Iyela, Ruanda, Sinde, Maanga na Ilemi na katka msako huo wamekamatwa watuhumiwa wawili [02] kwa makosa ya kupatikana na gongo/bhangi ambao ni AMINA KABALE [42] mkazi wa Mtaa wa Ilembo akiwa na lita 02 za gongo na HASSAN NASSORO [25] mkazi wa Tunduma akiwa na bhangi gramu 10.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho America, Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata MSAFIRI JACKSON [30] mkazi wa Nsalaga akiwa na bhangi gramu 10 kwenye mfuko wa suruali. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho America kilichopo Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Askari Polisi walimkamata AUGUSTINO MAHINYA [24] mkazi wa Nsalaga akiwa na bhangi gramu 10 kwenye mfuko wa suruali. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO]
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho shimoni kilichopo Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata NAOMI SAID [43] mkazi wa Uyole ya kati akiwa na lita kumi [10] za gongo. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO]
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:40 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho shimoni, kilichopo Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata LAZACK MWAKABUNGU [61] mkazi wa Uyole ya kati akiwa na lita kumi na tano [15] za gongo. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 16:00 jioni huko mtaa wa Mwasote, Kata ya Itezi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata RAHIM MABLUKI, [18] mkazi wa Nsalaga akiwa na bhangi uzito wa gram 25 kwenye mfuko wa suruali yake. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumaji wa bhangi.

Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi wa mashauri yao kukamilika.
 
Imetolewa na:
[ULRICH OMATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )