Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 28, 2020

Joseph Selasini (CHADEMA) Aimwagia Sifa Serikali....Wabunge CCM Walipuka kwa Shwangwe

juu
Pongezi kwa Serikali  zilizotolewa na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini bungeni mjini Dodoma zimeibua shangwe kutoka kwa wabunge wa CCM.

Mbunge huyo ambaye hivi karibuni alijiuzulu kuwa  kaimu mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ameipongeza Serikali leo Jumanne Januari 28, 2020 alipokuwa akiuliza swali  la nyongeza kuhusu upatikanaji wa maji wilayani Rombo.

Selasini amesema hivi sasa katika jimbo lake maji yanatokana hivyo akaishukuru Serikali.

"Kwa awamu zote za Serikali na wabunge walionitangulia wamekuwa wakitaka ziwa Kyara litumike kama chanzo cha maji lakini haikuwezekana, lakini Serikali hii naipongeza imewezesha," amesema Selasini.

Awali,  naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imepanga kutumia chanzo cha maji cha ziwa Kyara kufikisha maji Rombo, kwa kuanza  inapeleka Sh1.5 bilioni.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )