Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 23, 2020

Kangi Lugola Amkwaza Rais Magufuli...." Hamfai kwenye Hizi Nafasi na Sikutegemea Kuwakuta adi sasa"

adv1
Rais Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias  Andengenye hawafai kuendelea na nyadhifa zao kutokana na mambo waliyoyafanya.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa nyumba 12 za Askari Magereza kwenye Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kulikuwa na mkataba ambao ni wa ajabu.

“Kazi ya uongozi ni ngumu sana tuna changamoto nyingi, kama kuna wizara inanitesa ni hii ya mambo ya ndani tangu tumeingia madarakani katika kipindi cha miaka minne kuna tume zimeundwa kwaajili ya kuichunguza wizara hii kwa miradi ya hovyo iliyokuwa ikifanyika na nilitegemea watu watakuwa wanajifunza, tatizo kubwa ni watu kukosa uadilifu

“Hivi karibuni palikuwa na mkataba wa ajabu unatengenezwa Wizara ya Mambo ya Ndani wenye dhamani wa Euro milioni 408 na mradi huo umetayarishwa na kusainiwa na Kamishna Jerenali wa fire haujapangwa kwenye bajeti wala kupitishwa na bunge, wakati wa vikao na kampuni moja nafikiri kutoka Romania wahusika wote wa watanzania waliokuwa wanakwenda kwenye majadiliano wanalipwa ‘sitting allowance’ ya Dola 800 bado ya kulipiwa kwenye tiketi za ndege wakausaini mradi wa hovyo lakini masharti yanasema ukitaka kuuvunja yale ambayo yameshaanza kutekelezwa lazima yaendee kutekelezwa

“Mimi ninampenda sana Kangi Lugola ni mwanafunzi wangu nimemfundisha pamoja na mwili wake na ukubwa wake lakini kwenye hili hapana nilitegemea hata hapa nisingemkuta hatuwezi kuendesha nchi kwa misingi ya ajabu namna hii yanayokwenda kununuliwa kule kwenye mkataba ni ya ajabu mno

“Ninashangaa kuwaona Kangi Lugola na Kamishana Jenerali bado mko hapa sitaki kuwa mnafiki mtu anasaini zaidi ya Sh trilioni moja wakati sheria zote zinajulikana mwenye mamlaka ya kukopa fedha kwaajili ya Tanzania ni Wizara ya Fedha peke yake ikiwa hivyo kila mtu atakuwa anakopa hata mimi nitakopa sasa mimi nitaendelea kuwapenda lakini kwenye position hii no

“Watanzania mlinichagua kwaajili ya kuja kusimamia haki na utendaji ndani ya serikali ili kila fedha inayochangwa itumike kwa mujibu wa sheria na ndio maana mtaona miradi hii inatokea ni kwasababu tumebana na tunataka miradi yote iende kwa mujibu ilivyopangwa kwahiyo saa nyingine msisikitike sana mkimuona mnamuonea huruma ili kusudi akajifunze vizuri huo ndio ukweli na siku zote nitasimamia ukweli

“Wale wote waliofanikiwa kupata madaraka yawe ya kuteuliwa na mimi au na wasaidizi wangu watambue wana jukumu moja la kuwafanyia kazi Watanzania na bahati nzuri wengi wanafanya vizuri sasa yule atakayekuwa anajikwaa iwe ni kwa makusudi au bahati mbaya ukianguka ukajipange vizuri ili baadae usimame

“Urafiki, upendo bado uko pale pale lakini katika suala la kazi no way, tha’s me kwahiyo tusubiri wakati utakapokuja kwa wale watakaoona unafanya lolote waakakuangalia tu basi utakuwa utawala wa namna hiyo lakini utwala wangu hapana mimi ninataka watu wafaidi kweli kweli na ndio maana ninasema nitaendelea kuwa mtumishi kwahiyo Lugola ninakupenda sana umenisifia sana hapa lakini kwenye hili hapana sitaki kuwa mnafiki,” –Amesema Rais Magufuli
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )