Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 4, 2020

Maelfu wakusanyika kwa Maombolezo ya Kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani

Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika leo Jumamosi mjini Baghdad  kushiriki maandamano ya mazishi ya kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani, aliyeuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Marekani siku ya Ijumaa.

Wengi wa waombolezaji walivalia nguo nyeusi na kubeba bendera za Iraq pamoja na bendera za wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ambao ni watiifu kwa jenerali Soleimani. 

Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika oparesheni ya Iran Mashariki ya kati na taifa hilo limeapa "kulipiza kisasi" mauaji yake.

Waandamanaji walianza kukusanyika mjini Baghdad mapema asubuhi ya Jumamosi wakipeperusha bendera ya Iraq naya waasi wakiimba "kifo kwa Amerika".

Waandamanaji walizunguka barabara za mji huo wakibeba mababgu yaliyo na picha ya Soleimani huku wengine wakiwa na mabangu yaliyo na picha ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

Soma hii: Nafasi Mpya za Kazi Tanzania-January 2020

Ripoti zinasema mwili ya raia huyo wa Iran aliyeuawa katika shambulio hilo utasafirishwa nchini humo Jumamosi jioni, ambako siku tatu ya maombolezo imetangazwa kwa heshima ya jenerali.

Mazishi yake yatafanyika siku ya Jumanne nyumbani kwake Kerman eneo la kati la Iran.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )