Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 19, 2020

PICHA: Waziri Wa Viwanda Innocent Bashungwa Atembelea Kiwanda Cha Kuunganisha Mabasi Cha BM Motors Kilichopo Kibaha

juu
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa  amefanya ziara ya kikazi ya siku moja Halmashauri ya Mji Kibaha na  kutembelea kiwanda cha kuunganisha mabasi cha BM Motors kinachomilikiwa na Mtanzania chenye uwezo wa kuunganisha mabasi makubwa yenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 50.


Katika ziara yake jana Mjini Kibaha, Waziri Bashungwa akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Riziki Shemdoe, alieleza namna alivyoridhishwa na halmashauri hiyo inavyotekeleza sera ya uwekezaji wa viwanda kwa vitendo.

Akiwa katika kiwanda cha kuunganisha mabasi makubwa kinachomilikiwa na Kampuni ya BM Motors, alimpongeza mwekezaji wa Kitanzania kwa uwekezaji wake wenye tija.

Alisema, kitendo cha mwekezaji huyo mzawa kuwekeza hapa nchini, ni manufaa kwa Taifa katika suala la kodi, ajira kwa Watanzania, lakini ni fursa kwa viwanda vingine kwani malighafi zinazotumika zinapatikana nchini.

Mbali ya kiwanda hicho, Waziri Bashungwa pia alitembelea kampuni ya wawekezaji wazawa ya GF Vehicle Assemblies kilichopo eneo la Tamco.

Kampuni hiyo ambayo inatarajia kuanza kuunganisha magari mchanganyiko yenye uzito usiozidi tani nane, uzinduzi wake unatarajia kufanyika Mei mwaka huu.

Bashungwa aliwapongeza wawekezaji waliowekeza nchini, huku akitoa rai kwa mamlaka na taasisi zinazohusika na viwanda vidogo vidogo zikiwamo SIDO, DIT na NEMC kuwa karibu na wawekezaji kwa ushauri wa kitaalamu.

ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )