Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 11, 2020

Vikosi vya Syria vyakamata barabara muhimu kaskazini magharibi mwa Nchi hiyo

juu
Serikali ya Syria na vikosi vya washirika hii leo vimelikomboa eneo la mwisho la barabara moja kuu kutoka mikononi mwa waasi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. 

Hii ni baada ya miezi kadhaa ya mashambulizi kwenye ngome ya waasi ya Idlib na ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 2012 ambapo serikali imeidhibiti barabara nzima ya M5, ambayo inaunganisha mji mkuu Damascus na miji mingine muhimu kama vile Hama, Homs na Aleppo.

 Mkuu wa Shirika linalofuatilia Haki za Binaadamu nchini Syria Rami Abdel Rahman amesema serikali imelikomboa eneo la Rashideen al-Rabea katika mkoa wa Aleppo. 

Utawala wa Rais Bashar al-Assad ulipoteza maeneo makubwa ya nchi hiyo kwa waasi kutokana na mzozo huo uliozuka kufuatia  maandamano ya kuipinga serikali mwaka wa 2011.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )