Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 22, 2020

Wanajeshi Waliojeruhiwa Kwenye Shambulizi la Makombora la Iran Wafika 110

juu
Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa idadi ya wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa katika shambulizi la kombora la Iran kwenye kambi yake nchini Iraq mwezi uliopita imefikia 110. 

Idadi hiyo ni ya juu zaidi kuliko ile iliyotangazwa Februari 10. Taarifa ya wizara hiyo imesema wanajeshi wote waliojeruhiwa waligundulika kuathirika kwenye ubongo pamoja na kuwa na msongo wa mawazo. 

Kwa mujibu wa wizara hiyo, wanajeshi 77 tayari wamesharejea kazini. 

Wakati huo huo, wanajeshi 35 walipelekwa Ujerumani kwa uchunguzi zaidi, na 25 kati yao walipelekwa Marekani.

 Awali, Rais Donald Trump alisema kwamba hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo lililotokea kwenye kambi ya jeshi ya Ain al-Asad magharibi mwa Iraq usiku wa Januari 7 na 8. 

Hata hivyo, maafisa waliripoti kuwa wanajeshi kadhaa walijeruhiwa.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )