TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA WATUHUMIWA WANNE WA WIZI WA MABILIONI YA BENKI YA NBC JIJINI DSM
______________________
KUKAMATWA WATUHUMIWA WANNE WA WIZI WA MABILIONI YA BENKI YA NBC JIJINI DSM
______________________
Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu wanne
waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya G4S Security kwa tuhuma za
wizi wa Tsh 1.280,000,000/=,USD402,000 na Euro 27,700. Watuhumiwa hao ni;
1. CHRISTOPHER CLEOPHACE RUGEMALILA (34) dereva wa G4S, mkazi wa Chanika
2. MOHAMEDI ATHUMANI RAMADHANI (40) mlinzi G4S, mkazi wa mtoni kijichi
3. IBRAHIMU RAMADHANI MAUNGA (49), Mlinzi G4S, mkazi wa kiluvya.
4. SALIMU SHAMTE (45) mkazi wa Mbagala kizuiani.
Mnamo tarehe 07/02/2020 watuhumiwa watatu ambao ni
CHRISTOPHER RUGEMALILA, MOHAMEDI ATHUMANI na IBRAHIMU MAUNGA wakiwa na
gari namba T 728 BAN, NISSAN HARD BODY, mali ya kampuni ya G4S, Gari la kusindikiza fedha.
Walinzi hao walikabidhiwa fedha kutoka tawi la benki ya NBC Kariakoo na
NBC samora ili wazipeleke makao makuu ya benki ya NBC yaliyopo posta ya
zamani sokoine drive, lakini hawakufanya hivyo, matokeo yake walipanga
njama na kuelekea maeneo ya Temeke Maduka mawili karibu na kituo cha
mafuta cha CAMEL na kuchukua fedha zote na kupakia kwenye gari ndogo
T.134 DHY Toyota IST ikiendeshwa na SALUMU SHAMTE. Watuhumiwa hao
baada ya kufanikisha uhalifu huo walitelekeza gari la Kampuni ya G4S,
silaha mbili mali ya G4S, moja aina ya pump action, na bastola moja,
mashine ya kuhesabia fedha na muhuri wa Benki ya CBA kisha kuondoka
kusikojulikana.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam baada ya kupata taarifa
hizo liliunda kikosi kazi na kuanza ufuatiliaji mara moja, ambapo tarehe
17/02/2020 majira ya mchana huko Mongo la ndege Mtuhumiwa wa kwanza
aitwaye CHRISTOPHER CLEOPHACE RUGEMALILA alikamatwa na alipopekuliwa
alikutwa na Tsh 110,000,000/= USD 19,000 zikiwa ndani ya gari lake T 691
BMW DSU, Magari matano yenye namba za usajili, kama ifuatavyo;
- T691DSU BMW yenye thamani yake Tsh 15,000,000/=
- T909DSU Toyota Runx yenye thamani Tsh 13,000,000/=
- T627DSU Toyota IST yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
- T653DSU Toyota IST, yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
- T857DSU Toyota IST. yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
Mtuhumiwa baada ya kuendelea kuhojiwa alikiri tayari ameshanunua
nyumba mbili na kiwanja kimoja vyenye thamani ya TSH 107,000,000/=
samani za ndani vyenye thamani ya Tsh 5,000,000/= na kufanya jumla ya
mali na fedha taslimu Tsh 297,110,000/= USD 21,000.
Tarehe 21/02/202 watuhumiwa wawili walikamatwa MOHAMED RAMADHANI na
SALIMU SHAMTE huko Mbagala na walipopekuliwa walikutwa na Tsh
332,000,000/= USD 50,000, EURO 5010 na GARI T134 DHY Toyota IST
iliyotumika kubebea fedha baada ya kuiba na kutelekeza gari la kampuni
ya G4S.
Watuhumiwa wote wawili baada ya mahojiano walikiri kununua viwanja
viwanja viwili maeneo ya kisemvule na kivule vyenye thamani ya Tsh
25,000,000/=. Jumla kuu ya mali na fedha taslimu ni Tsh 357,000,000/= USD 50,000 na EURO 5010
Aidha upelelezi uliendelea na tarehe 24/02/2020 mtuhumiwa IBRAHIMU
RAMADHANI MAUNGA alikamatwa na baada ya kupekuliwa alikutwa na Tsh
195,213,450, USD 70,600, nyumba aliyonunua kibaha Tsh 30,000,000/= na
samani za ndani zenye thamani ya Tsh 10,000,000/=
Jumla kuu ya mali na fedha ni Tsh 253,000,000/=
Jeshi la polisi kanda maalum limefanikiwa kukamata watuhumiwa wote
watatu pamoja na mtuhumiwa mmoja ambaye aliwasaidia kukamilisha wizi
huo.
Sambamba na hilo, tunawashikilia askari Polisi tisa kwa kukiuka maadili ya kazi wakati wa ufutiliaji na upekuzi wa tukio
hili.
KUUWAWA KWA JAMBAZI SUGU JIJINI DSM
Katika
tukio la pili, mnamo tarehe 24/02/2020 majira ya saa saba na nusu usiku
huko maeneo ya saba saba mbagala kizuiani, kikosi kazi cha kupambana na
majambazi kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa RAMADHANI RASHIDI @ASNEY
MJEURI (20) mkazi wa mbagala, mtuhumiwa huyo wakati mahojiano alikiri
kujihusisha na tuhuma mbalimbali za ujambazi maeneo ya TOANGOMA, Mbagala
na Mkuranga. Ndipo alikubali kwenda kuwaonyesha askari alipoficha
silaha na watuhumiwa anaoshirikiana nao na walipofika eneo hilo alianza
kukimbia huku akipiga kelele na askari walifyatua risasi tatu hewani
kumuamuru asimame lakini mtuhumiwa huyo aliendelea kukimbia na ndipo
alipopigwa risasi mgongoni na kufariki dunia.
LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
25/02/2020
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
25/02/2020
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )