Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 19, 2020

Waziri Mkuu Anatarajia Kuwasili Mkoani Kagera Kwa Ziara Ya Siku Mbili.

juu
Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassimu Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku mbili katika mkoa wa Kagera yenye lengo la kufanya shughuri za chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na Serikali.
 
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa  wa Kagera Brigedia  Jenerali Marco Elisha Gaguti wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mnamo tarehe 19/02/20209, na kuongeza kuwa, Mh Majaliwa anatarajia kuwasili mkoani humo mnamo tarehe 20/02/2020 saa 03:30 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Bukoba.
 
Ameongeza kuwa katika ziara yake  ya siku mbili mh Majaliwa atapata taharifa ya mkoa  pamoja na kukagua shughuri za Chama Cha Mapinduzi(CCM)  ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi wa chama ndani ya Mkoa ikizingatiwa kwamba yeye ndiye mlezi wa Chama Cha Mapinduzi  mkoani humo.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )