Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 13, 2020

Halima Mdee, Ester Bulaya, Boniface Jacob Wakamatwa Wakijiandaa Kumtoa Mbowe Gerezani

juu
Wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee na Ester Bulaya, Meya wa Ubungo Boniface Jacob, Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar, Henry Kileo na wanachama wengine wamekamatwa na polisi baada ya kutokea vurugu wakati wakifuatilia Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  kutolewa katika gereza la Segerea.

Mdee na Bulaya walitoka jela jana baada ya kulipa faini, leo walikwenda kumpokea Mbowe ambaye amekamilisha taratibu za kutoka jela.

Viongozi hao wamekamatwa saa 7:30 mchana baada ya kufika katika gereza hilo na kuanza kuzuiwa na askari wa Jeshi la Magereza waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.

Wakati mabomu hayo yakipigwa, viongozi hao wa Chadema waliwekwa chini ya ulinzi kwa madai ya kukiuka amri halali ya kuwataka kuondoka katika eneo hilo.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )