Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 9, 2020

Korea Kaskazini yarusha makombora matatu katika Bahari ya Mashariki

Korea kaskazini imefyatua leo silaha zisizojulikana, na kusababisha hali ya wasi wasi katika rasi ya Korea. 

Mkuu wa majeshi ya Korea kusini amesema vitu hivyo vilifyatuliwa katika upande wa mashariki baharini kuelekea Japan. 

Mkuu huyo wa majeshi amesema jeshi linaangalia iwapo kutakuwa na ufyatua zaidi na kujiweka tayari. 

Korea Kaskazini imo katika shinikizo linaoongezeka la kimataifa kusitisha mpango wake wenye utata wa silaha, ikiwa ni pamoja zile zenye lengo la kutengeneza silaha za maangamizi na jinsi ya kuzitumia.

 Mwezi Desemba, kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un alisema nchi yake haifungwi tena hatua ya kusitisha kwa muda mpango wake wa kinyuklia pamoja na mpango wa makombora ya masafa marefu. 

Mazungumzo kati ya Korea kaskazini na Marekani yenye nia ya kuondoa silaha katika eneo la rasi ya Korea yameendelea kukwama baada ya mkutano kati ya Kim na rais wa Marekani Donald Trump kuvunjika mwaka jana. 

Wiki iliyopita , Korea kaskazini ilifyatua makombora mawili ya masafa ya mafupi, na kusababisha shutuma kutoka jumuiya ya kimataifa.

-DW
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )