Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 6, 2020

Urusi, Uturuki Zakubaliana Kusitisha Mapigano Idlib nchini Syria

juu
Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kati ya rais Vladimir Putin wa Uurusi na Recip Tayyip Erdogan wa Uturuki yameanza kutekelezwa usiku wa manane leo katika jimbo la Kaskazini Magharibi ya Syria la Idlib.

 Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria limesema kumekuwepo utulivu kwenye maeneo mengi yaliandamwa na mapigano kwa wiki kadhaa zilizopita. 

Hata hivyo, duru zimearifu kuwa muda mfupi kabla ya kuanza usitishaji mapigano ndege za kivita za Urusi na makombora ya jeshi la Syria yaliushambulia mji wa pembezoni wa Hama. 

Wakati huo huo Uturuki imeripoti kuwa imewauwa wanajeshi 21 wa Syria na kuharibu mifumo minne ya kufyetua makombora baada ya wanajeshi wake wawili kuuwawa. 

Mapema jana wanajeshi wawili wa Uturuki walikufa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya jeshi la Syria kuushambulia mji wa Idlib.

-DW
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )