Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 3, 2020

Kamati Ya Bunge Ya Bajeti Yashauri Kampuni Za Simu Kujiorodhesha Kwenye Soko La Hisa Dsm Ili Watanzania Waweze Kushiriki Uwekezaji Katika Sekta Ya Mawasiliano.

juu
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kamati  ya  Bunge ya bajeti  imeshauri kampuni za simu ambazo bado hazijaorodheshwa kwenye soko la Hisa la Dar es salaam waweze kufanya hivyo ili Watanzania waweze kushiriki katika uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano kama sheria inavyotoka.

Hayo yamebainishwa Bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Mashimba Mashauri Ndaki wakati akiwasilisha  taarifa ya mwaka kuhusu utekelezaji wa majukumu ya kamati ya bunge ya bajeti katika kipindi cha mwezi januari, 2019 hadi mwezi januari, 2020 pamoja na tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa kipindi cha nusu mwaka julai - Disemba 2019.

Mhe.Mashimba amesema Utekelezaji wa Sheria ya Mawasiliano na Kielektroniki (EPOCA ]Marekebisho yaliyofanyika kwenye Sheria ya EPOCA mwaka 2017, yalielekeza kampuni zote za simu kujiorodhesha kwenye soko la hisa na kuuza asilimia ishirini na tano (25%) ya hisa zake kwa umma na hatimaye kampuni hizo kuorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es salaam.

 Hata hivyo, Kamati ilibaini kuwa kati ya kampuni zote za simu ni kampuni ya Vodacom tu ambayo imeweza kuingia kwenye soko , Pamoja na kuwa Vodacom wameingia sokoni sio hisa zote ambazo zimeweza kununuliwa na inalamikiwa kutoa gawio dogo lakini pia kushuka kwa thamani ya hisa za kampuni hiyo hivyo kuna wajibu wa kampuni zote za mawasiliano kujiorodhesha kuingia kwenye soko la Hisa Dar Es Salaam hali itakayosaidia watanzania kushiriki uwekezaji katika sekta ya Mawasiliano.

Kuhusu Sekta ya Ngozi Mhe Ndaki amesema , wakati wa kujadili Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 Kamati ilipokea Taarifa kutoka kwa wafanyabiashara wa ngozi kuhusu mlundikano wa ngozi katika maghala uliosababishwa na viwango vya ushuru wa mauzo nje yaani export levy ya asilimia 10 kwa ngozi zilizosindikwa hadi hatua ya wet blue na asilimia 80 kwa ngozi ghafi, viwango 29 ambavyo vilipelekea ngozi kukosa soko.

Hivyo, Serikali iliahidi kulifanyia utafiti suala hilo na kuwasilisha Taarifa kwenye Kamati ambapo Matokeo ya tafiti uliofanywa na Serikali yalibaini kuwepo na mlundikano wa ngozi katika maghala ambayo yalifanyiwa utafiti katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Mwanza na Kilimanjaro.

Kutokana na hilo Kamati inaiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakishirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kufanyia utafiti viwango hivyo vya ushuru na kuangalia ni namna gani zinaweza kuja na mikakati ya kusaidia na kuinua sekta hiyo ambayo ina manufaa makubwa ya kimapato kwenye uchumi wa nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria  Mhe.Mohammed Omary Mchengerwa amesema kamati yake imeridhishwa na Mradi wa Program ya Kukuza ujuzi nchini ambao ulitengewa Bilioni 18.

Mhe.Mchengerwa amesema pamoja na Kamati kuridhishwa na jinsi Hazina ilivyotoa  kwa wakati Fedha za kuiwezsha Tume ya Uchaguzi kuboresha Daftari la Wapiga kura, bado Kamati inaendelea kuishauri Serikali kuhakikisha inatoa Fedha zinazoidhinishwa na Bunge  kwa Wakati ili kuiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuratibu masuala mbalimbali ya Uchaguzi kwa ufanisi Mkubwa.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )