Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, May 30, 2020

Kansela Angela Merkel akataa kuhudhuria mkutano wa G7 Marekani

juu
Kansela Angela Merkel amekataa kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la nchi 7 zenye uchumi wa juu zaidi duniani, G7, nchini Marekani mnamo mwezi Juni, kama ilivyopendekezwa na rais wa Marekani, Donald Trump.

Angela Merkel amesema hatohodhuria mkutano huo, kwa sababu ya janga la Corona, msemaji wa serikali ya Ujerumani amelithibitishia shirika la habari la AFP leo Jumamosi.

"Kwa leo, ukizingatia hali ya jumla ya janga la Corona, hawezi kukubali kusafari kwenda Washington," amesema msemaji wa serikali ya Ujerumani, akithibitisha habari ya chombo cha habari mtandaoni cha Politico kutoka Marekani.

"Ofisi ya kansela wa Ujerumani inamshukuru rais Trump kwa mwaliko wake kwenye mkutano wa G7," msemaji wa serikali ya Ujerumani ameongeza.

Bi Merkel, ndiye kiongozi wa kwanza wa kundi la G7 (Japan, Canada, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia) kukataa rasmi mwaliko huu.

Umri wa Merkel, 65, ambaye pia ni sawa na ule wa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, unamweka katika hatari kubwa ya kuambukizwa haraka janga la Covid-19.

Marekani ni nchi ya kwanza kuathirika zaidi duniani (zaidi ya watu 100,000 wamefariki dunia kwa Covid-19, huku watu Milioni 1.7 wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo).

Ikulu ya White ilikuwa imetangaza mwanzoni mwa mwezi Machi kuwa inasitisha maandalizi ya mkutano huo, kwa sababu ya janga la Corona, kwa kuwaleta pamoja marais na viongozi wa serikali kutoka n-kundi la G7, ingependelea mkutano huo ufanyike kupitia video.

Lakini wiki iliyopita, Donald Trump alitangaza kwamba mkutano wa kilele wa kundi la G7 utafanyika mwezi wa Juni "katika Ikulu ya White House", ingawa kuna mikutano kadhaa ambayo inaweza kufanyika katika makazi ya rais ya Camp David, katika jimbo jirani la Maryland.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )