Idadi ya maambukizi ya corona nchini Kenya imefikia watu 1618, hii ni baada ya watu 147 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita baada ya sampuli 2831 kufanyiwa uchunguzi.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuwa miongoni mwa maambukizi hayo mapya 147, 90 ni jijini Nairobi na 41 ni huko Mombasa.
Vilevile idadi ya waliofariki imefikia 58 baada ya watu wengine watatu kufariki,wawili huko Mombasa na mmoja huko Kiambu.
Idadi ya waliopona imefikia 421 baada ya watu 13 zaidi kupona na kuondoka hospitalini.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )