Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, May 31, 2020

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Nane (08)

juu
Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA
Akaning’inizwa hewani huku mikono yake ikiwa imechanuliwa mithili ya Yesu alivyo sulubiwa msalabani. Wapelelezi hao wakamwagia maji mwilini mwake, kisha mmoja wao ahachukua nyaya mbili za umeme, zenye hasi na chanya. Akazigusanisha na zikaanza kutoa cheche cheche, zilizo mfanya Tomas kujawa na mshangao hata kabla ya kupachikwa na nyaya hizo mwilini.
“Ukijibu kwa usahihi basi adhabu hii huto ipata. Ila ukijiu kwa jeuri basi adhabu hii utakumbana nayo.”
Kauli ya mpelelezi ikamfanya Tomas macho kumtoka huku akiwa haelewi ni kosa gani lililo mfanya kukumbana na shurba zote hizo.
“YUPO WAPI NABII SANGA”   
Mapigo ya moyo ya Tomas yakaanza kumdunda kwa kasi sana kwani hakutarajia kwamba, mpango wa siri alio upanga yeye na mrs Sanga utajulikana kirahisi namna hiyo.


ENDELEA
“Mi……mi sijui”
Tomas alizungumza kwa kubabaika. Kutokana na utaalamu walio nao wapelelezi hawa. Wakatambua kabisa jibu la Tomas si la kweli. Mpelelezi aliye shika nyaya hizo za umeme, akazipatichika kwenye mbavu za Tomas na kumfanya aanze kutetemeshwa huku akipiga mayowe makubwa yatokanayo na maumivu hayo makali sana.
“Ni wapi mulipo muhifadhi nabii Sanga?”
“Nitasema nitasema”
Tomas alizungumza huku machozi yaliyo ambatana na mkojo vikianza kumchurukika kwa pamoja.
                                ***
“Hapa panatosha. Chukua hii kofia uvae ili watu wasiweze kukugundua.”
Rama D alizungumza huku wakilisimamisha gari lao karibu kidogo na stendi ya Mkinga. Nabii Sanga akachukua kofia nyeusi aliyo pewa na akaivaa.
“Hakikisheni kwamba muna fanya kile nilicho waeleza muweze kufanya”
“Sawa tutafanya hivyo”
Magreth akafunguliwa kitambaa machoni mwake na wakashuka na nabii Sanga kwenye gari hilo. Rama D na wadogo zake wakawasha gari na kurudi porini huku wakiwa wamejawa na furaha ya kupata kiasi kikubwa sana cha pesa.
“Upo salama baba?”
Magreth aliuliza huku akimtazama nabii Sanga mwilini mwake.
“Ndio. Ulicho kiona na ulicho kisikia hakikisha umuambii mtu”
“Sawa baba sinto fanya hivyo”
“Inabidi tutafute usafiri wa kurudi Dar”
“Nimekuja na dereva taksi, acha niwasiliana naye”
Magreth akampigia Sheby, baada ya sekunde kadhaa Sheby akapokea simu.
“Sheby, mimi Mage”
“Niambie upo wapi?”
“Nipo karibu na sheli hapa stendi”
“Poa ngoja nina kuja hapo kwa maana nilikuwa nimepitiwa na ka usingizi”
“Poa poa”
Sheby akawasha gari lake na kuelekea eneo ilipo sheli na kuwakuta Magreth na mwanaume ambaye hakuweza kumfahamu, hii ni kutokana na uvaaji wake wa kofia ulio ificha sura yake. Wakaingia kwenye taksi hiyo, na wote wawili wakakaa siti ya nyuma.
“Tunarudi Dar ehee?”
Sheby alizungumza huku akitazama nyuma kwa kupitia kioo kilichopo pembeni yake.
“Ndio”
Magreth alijibu kwa ufupi.
“Poa”
Safari ikaanza huku ndani ya gari ukimya ukitawala. Nabii Sanga hakutamani hata kufungua kinywa chake, hii ni kuhofia sauti yake kujulikana na dereva taksi huyo. Majira ya saa saba usiku wakaingia jijini Dar es Salaam. Moja kwa moja wakaelekea nyumbani kwa Magreth.
“Hivi Sheby ni wapi sasa hivi watakuwa hawajafunga vibanda vya chipsi?”
“Zipo sehemu nyingi mbona”
“Basi ngoja nimpeleke mgeni wangu ndani. Nisubiri hapa tukachukue wote”
“Sawa bossi”
Magreth na nabii Sanga wakashuka kwenye gari hilo na kuingia ndani ya nyumba hiyo iliyopo uswahilini. Magreth akafungua mlango wa chumbani kwake na wakaingia ndani, pasipo mpangaji mwezake yoyote kugundua juu ya ugeni wa nabii Sanga.
“Hapa ndio kwangu jisikie huru”
“Nashukuru Magreth”
“Basi ngoja nikachukue chakula. Si unatumia chipsi za huku kwetu”
“Una maanisha nini ukisema huku kwenu?”
“Uswahilini, si unajua kuna utaofauti na zile chipsi za kwenye migahawa mikubwa mikubwa?”
“Wewe lete chakula chochote nitakula”
“Sawa”
Magreth akaliweka begi lake sehemu alipo litoa, kisha akatoka ndani humo na kurudi kwenye taksi.
“Mage wewe muongo”
“Kwa nini?”
“Uliniambia kwamba huna mtu”
“Hembu kumbuka vizuri”
“Ndio, nilikuuliza tunakwenda Mkinga kwa jamaa yako. Ukasema hapana, ona sasa umerudi na mtu wako. Yaani umenifanya njia nzima nikae kimya nishindwe hata kupiga stori”
“Hahaa woga wako tu.Twende bwana tukachukue chakula”
Magreth na Sheby wakaondoka eneo hili na kuelekea kwenye kibanda cha Masawe anaye sifika kwa kupika chipsi nzuri sana na ana wateja wengi wanao mfanya kila siku afunge kibanda chake saa kumi usiku au saa kumi na moja alfajiri.
“Na wewe uta kula chipsi na nini?”
Magreth alimuuliza Sheby anaye onekana kuchoka kiasi fulani.
“Chipsi kuku”
“Nakununulia wewe na mke wako. Hakikisha mtoto wa watu unampeleka hichi chakula. Nina imani atakuwa amekupigia simu urudi nyumbani ukale, ila ndio hivyo ulikuwa mbali”
“Sawa mama”
Magreth akashuka kwenye gari hilo, kutokana ana fahamiana na Massawe. Ikamuwia urahisi kuhudumiwa kwa haraka na kuondoka. Wakarudi nyumbani, Magreth akamuongezea Sheby kiasi cha shilingi elfu ishirini, wakaagana na yeye akaingia ndani.
Magreth akastuka kidogo mara ya kumkuta nabii Sanga akiwa na boksa tu huku amelala chali kitandani. Nabii Sanga aliye jawa na mawazo kichwani mwake, kumemfanya asitambue uwepo wa Magreth ndani humo. Magreth aliye anza kupepesa macho akijikaza asimtazame nabii Sanga. Akamsogelea na kushika mkono na nabii Sanga akastuka kidogo.
“Nimerudi.”
“Ohoo sawa sawa”
Magreth akachukua taulo na kumkabidi nabii Sanga huku akiwa ametazama pembeni. Kwani haitaji kabisa kuona maungo ya chini ya mtu anaye muheshimu kama baba yake. Nabii Sanga akajifunga taulo hilo na kumpa amani Magreth.
“Toka jana sikuweza kutia kitu chochote mdomoni mwangu”
“Pole sana baba”
“Mage”
“Bee”
“Ukiwa nami naomba usiniite baba wala nabii”
“Aha…a…ha…Kwa nini?”
“Niite tu Sanga peke yake, sinto pendelea ukitese kinywa chako kwa kuita jina refu”
“Ila baba hivi ndivyo nilivyo zoea na ninakupa cheo chako kutokana na mambo makubwa ambayo Mungu ana endelea kutufunulia juu yako”
“Sawa nina litambua hilo, ila tafadhali fanya hivyo nilivo kueleza”
“Nitajitahidi”
Magreth akaandaa chakula na wote wakaanza kula huku nabii Sanga kwa mara kadhaa ana endelea kutazama uumbaji wa Mungu alio ufanya juu ya Magreth. Ila Magreth kichwani mwake ana waza ni jinsi gani ambavyo anaweza kumkabidhi nabii Sanga ushahidi wa video unao onyesha uchafu wa mke wake pamoja na Tomas.
                                ***
Tomas hakutamani nyaya hizo ziweze kurudishwa tena mwilini mwake. Ila kitu cha pekee ambacho ana jitahidi kukificha ni ushirikiano wake na mrs Sanga.
“Ni wapi?”
Mpelelezi huyo alimuuliza Tomas kwa upole huku akimtazama usoni mwake. Kabla ya Tomas kujibu RPC akaingia katika chumba hicho, huku akiwa ameongozana na body gard wake.
“Mume fikiwa wapi vijana?”
“Ana hitaji kutaja ni wapi walipo wezake.”
“Tunakusikiliza wewe kenge. Sema wapi alipo nabii Sanga?”
RPC alizungumza kwa ukali na kumfanya Tomas kuanza kuzungumza ni eneo gani walipo wezake.
“Wasiliana na RCO wa Handeni. Aniandalie vijana wanne, wakakamavu na wenye uwezo mkubwa. Nyinyi mutaongoza timu ya askari nane kuelekea msituni huko.”
“Sawa mkuu”
“Kamera mliyo piga picha ipo wapi?”
“Hii hapa mkuu”
“Nenda kazisafishe picha hizo sasa hivi”
RPC alimueleza body gard wake huku akiipokea kamera hiyo na kumkabidhi kijana wake.
“Sawa mkuu”
“Kikosi hicho hakikisheni kwamba nina onana nacho sasa hivi na wawe vijana mashupavu”
“Sawa mkuu acha nikiandae kikosi”
“Haya. Nahitaji kusikia mazungumzo ya mwisho ya huyu kijana aliyo yafanya kwenye simu yake. Niunganishe na kurugenzi wa mtando wa simu anao utumia ili tuweze kutumiwa mazungumzo yake ya mwisho”
“Sawa mkuu”
Tomas akashushwa kwenye minyororo hiyo huku mwili mzima ukiendelea kumtetemeka kwa woga na maumivu makali aliyo yapata.
    Akavalishwa nguo zake na kutolewa katika chumba hicho cha mateso na kuwekwa chumba cha mapumziko kabla ya kuchukuliwa na kuongozana na askai hao kuelekea Handeni.
RPC akazungumza na mkurugenzi wa mtandao wa simu anao utumia Tomas na akatumiwa mazungumzo ya mwisho na watekaji na ushahidi huo ukazidi kumuweka Tomas sehemu mbaya kisheria. Simu inayo pigwa kila mara kwenye simu ya Tomas kukamfanya RPC kuendelea kuzikata simu hizo kwani namba hiyo imeandikwa kwa jila na Mke wangu.
“Kijana mshenzi huyu ana mke alafu ana fanya mambo ya ajabu”
RPC alizungumza huku akiizima simu hiyo. Akaingia katika chumba cha silaha na kuwakuta vijana wake wakiwa wana jiandaa.
“Tusikilizane”
Kila askari akaacha kazi aliyo kuwa ana ifanya na kusimama wima mithili ya mlingoti ili kumsikiliza mkuu wao.
“Mna kwenda kwenye oparesheni hatari sana. Msitu huo ni mithili ya misitu iliyopo Kibiti. Hakikisheni kwamba mna kuwa makini sana kwa kila jambo ambalo mna lifanya.”
“Akikisheni mna muokoa nabii Sanga akiwa hai. Ila ombi langu ni moja tu. Musiache pumzi ya ya jambazi yoyote, hata ikitokea wame jisalimisha. Hakikisheni kwamba mna waua sawa”
“Sawa afande”
“Mtaongozana na huyo kijana Tomas. Hakikisheni mna rudi naye akiwa hai na gereza lita muhusu, ili iwe fundisho kwa vijana wengine wote. Udalali wake kumbe si kwenye nyumba tu, hadi kwa watu”
“Niwatakie kazi njema na mapambano mema”
“Shukrani mkuu”
Askari hao wakapiga saluti na RPC akatoka ndani humo na kuwaacha vijana wake wakiendelea kujiandaa. Kikosi hicho cha askari nane walio valia mavazi meusi, huku wote wakiwa wamejikamilisha kwa mapambano, wakaingia kwenye gari nne aina ya Toyota land cruzer zenye rangi nyeusi na kuianza safari ya kuelekea Mkinga, Handeni, huku Tomas akiwa miongoni mwa walio ndani ya magari hayo, tena chini ya ulinzi mkali sana.

                                ***
    Kitendo cha Tomas kuto kupoekea simu yake na kuizima kabisa, kikazidi kumchanganya Mrs Sanga. Namba yake ya siri aliyo iweka hewani, ndio anayo itumia kuwasiliana na Tomas.
“Amekumbwa na nini baby wangu?”
Mrs Sanga ali haha huku akiendelea kuzunguka zunguka ndani ya chumba hicho. Mlango wa chumbani kwake ukagongwa, akastuka sana huku akiutazama. Saa yake ya mkononi ina onyesha muda huu ni saa saba usiku.
“Nani?”
Mrs Sanga alizungumza huku akiutazama mlango huo.
“Ni mimi”
Sauti ya mkuu wa polisi wa kikosi kinacho mlinda yeye na familia yake, ikamstua sana. Mrs Sanga akajifunga tenge na kutoka ndani humo.
“Samahani mama kwa kukuamsha wakati huu”
“Bila samahani”
“Tunaweza kushuka sebleni mara moja”
“Kuna nini?”
“RPC yupo hapa”
“RPC!!?”
“Ndio”
“Sawa nina kuja”
Mrs Sanga akarudi ndani kwake huku mawazo ya kwa nini ameitwa muda huu yakiwa yamemtawala sana kichwani mwake. Akaitoa laini hiyo ya siri na kuiweka katika pochi yake. Akaweka laini yake ya kawaida. Akavaa suruli na tisheti kisha akatoka ndani humo. Akafika sebeleni na kumkuta RPC akiwa na vijana wake sita wenye bunduki. Uwepo wa mzee huyo kidogo uka mstua.
“Ahaa kwema jamani?”
Mrs Sanga aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Kwema, karibu unaweza kukaa tukazungumza mama”
RCP alizungumza huku akimkazia macho Mrs Sanga.
“Vijana wangu kwa sasa wapo njiani wana kwenda kwenye oparesheni ya kumkomboa mume wako. Tunashukuru sana kwa kuweza kutusaidia kumkamata mmoja wa watu walio mteka mume wako.”
Kauli ya RPC ikaufanya moyo wa mrs Sanga kumdunda mfululizo, huku moyo huo ukipoteza muelekeo wake wa kudunda.
“U…u…m….e…sema U…me….me..mkamata nani?”
Mrs Sanga alizungumza kwa kubabaika.
“Mtekaji wa mume wako.”
RCP akampa ishara kijana wake mmojaa kuweka bahasha ya rangi ya kaki, aliyo ishika mezani hapo.
“Fungua”
Mrs Sanga taratibu huku akitetemeka akaichukua bahasha hiyo. Akachungulia ndani ya bahasha hiyo na kukuta lundo la picha. Taratibu akazitoa picha hizo, Mrs Sanga alipo inaona sura ya Tomas akishuka kwenye gari lake, akahisi mwili mzima ukiishiwa nguvu, ubaridi mkali ukamtawala na kujikuta akiziangusha picha hizo na kuwafanya askari wote kumshangaa.
                            ITAENDELEA
Haya sasa, kitendo cha kuangusha picha hizo kitaleta picha gani kwa askari? Je Magreth ata weza kumpa nabii SANGA ushahidi wa video hiyo iliyomo kwenye simu yake? Nini kitatokea? Endelea kufaatilia kisa hiki cha kusisimua, usikose sehemu ya 09
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )