Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, June 14, 2020

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Ndumbaro Asaini Kitabu Cha Maombolezo Cha Rais Nkurunziza

juu
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini kufuatia kifo cha Rais wa Taifa hilo Pierre Nkurunziza aliyefariki Juni 08, 2020.

Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini, Jijini Dar es Salaam Dkt. Ndumbaro ametoa pole kwa wananchi wote wa Burundi na kuwasihi kuendelea kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu wa msiba.

"Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano wetu, umoja wetu na undugu wetu na ndugu zetu wa Burundi. Kifo cha Rais Nkurunzinza kinawahusu pia watanzania kwa sababu Rais Nkurunzinza ni Rais aliyekuwa karibu sana na Tanzania kuliko nchi nyingine yeyote ile, lakini pia Burundi ipo karibu sana na Tanzania, Amesema Dkt. Ndumbaro.

Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, Pengo la Rais Nkurunzinza ni pengo kubwa sana kwa watanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Afrika kwa ujumla.

Nae Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho, amemshukuru Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro kwa kufika kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaonesha upendo ambao unaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Aidha, Serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake hapa nchini, imetoa mualiko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kushiriki mazishi ya Rais Nkurunzinza yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi tarehe 18 Juni 2020 nchini Burundi.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )