Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, June 2, 2020

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Kumi (10)

juu
Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA
“Nawe pia mwanangu, ila ni vibaya kwa mtoto wa kike kulala chini huku mimi mwanaume niliye komaa nikilala kitandani. Huo utakuwa ni unyanyasaji mkubwa sana na nina weza nisipate usingizi kabisa mwanangu. Ninacho kuomba ni wewe uweze kulala kitandani na mimi uniache nilalale chini”
“Hapana baba wewe ni mgeni haina shinda. Wewe lala tu kitandani”
Magreth alizungumza huku akisimama, ila kwa bahati mbaya kitando cha nabii Sanga kumzuia katika kusimama kwake, kukapelekea tenge lake kulegea kishikizo alicho kuwa amekichomeka kifuani mwake na kupelekea tenge hilo kuanguka chini na kumfanya Magreth abaki kama alivyo zaliwa na kumfanya nabii Sanga ashuhudie uumbaji wa Mungu alio kuwa akiutamani kuuona siku zote mubashara.


ENDELEA
Magreth akahisi kama amepigwa shoti ya umeme, hakutamani hata siku moja maungo yake yaweza kuonakana mbele ya mwanaume ambaye hajawahi hata kumfikiria akilini mwake. Akainama kwa haraka na kulikota tenge hilo na kuanza kujifunga. Nabii Sanga akatakamani kuupeleka mkono wake wa kulia huku akiendelea kumeza mate ya uchu, ila akajikuta akishindwa kwani tayari Magreth amesha sogea mita kadhaa.
“Ahaa….nalala hapa chini”
Magreth alizungumza huku akijilaza chini. Ni asilimia chache sana ya wanaume ambao wana weza kuvumilia pale wanapo yaona maungo ya ndani ya mwanamke ambaye wana mtamani kwa kipindi kirefu. Nabii Sanga, akajikuta akisimama na kuvua taulo lake na kumfanya Magreth apigwe na butwaa, huku akimtazama jo wa nabii Sanga, jinsi alivyo kisawa sawa. Magreth kwa haraka akakurupuka chini hapo, kwani kwa kuendelea kujilaza kuna weza kumrahisishia nabii Sanga kukamilisha ushetani wake ambao tayari amesha anza kuudhihirisha mbele yake.
“Baba una fanya nini?”
Magreth alizungumza huku akiwa amerudi nyuma hadi ukutani.
“Mage natambua kwamba…..kwamba mimi pia ni binadamu. Nina hisia za kibinadamu. Tafadhali nina kuomba japo kidogo tu”
“Hapana baba, mimi ni mwanao tena mwanao wa kiroho, jifunge basi taulo lako.”
“Mage siwezi kuvumilia zaidi ya hapa, hembu tazama jinsi ... ilivyo . Tafadhali Magre nionee huruma”
Nabii Sanga alizungumza mithili ya mtu aliye changanyikiwa. Wadhifa, heshima yake ambavyo watu wengi wana mpatia vyote amevitupa pembeni. Magreth akazidi kushangaa mara baada ya kumuona nabii Sanga akipiga magoti chini huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Magreth usiku wa leo ukipita hivi hivi nina weza kufa. Ninaweza kufa Mage”
Nabii Sanga alilalama huku akiendelea kupiga magoti mbele ya Magreth ambaye ukifananisha hadhi zao ni sawa na mbingu na ardhi. Hapa ndipo ule usemi wa mapenzi hayanaga komando ndipo unapo chukua nafasi. Magreth kwa haraka akachanganua akili yake na kuikumbuka video ya ngono kati ya Mrs Sanga na Tomas. Akaichukua simu yake kwa haraka na kumfanya nabii Sanga kutokwa na macho.
“Mage una taka kunipiga picha hivi!!?”
“Hapana”
Magreth alijibu huku vidole vyake vikiwa na kazi ya kuchambua ni faili lipi lina video hiyo. Mara baada ya kuliona, akanyoosha mkono wake ulio shika simu na kumfanya nabii Sanga ashangae kidogo.
“Nini?”
“Tazama”
Nabii Sanga akaichukua simu ya Magreth, akaanza kuitazama video hiyo. Hamu ya kumtamani Magreth yote ikakata. Akasijikuta akikaa chini sakafuni huku akiwa uchi kabisa. Hasira na uchungu wa kuibiwa mke na mtu wake wa pembeni vikazidi kuutawala moyo na mwili wake.
‘Samahani nabii Sanga, sikupanga kukuonyesha video hiyo kwa wakati huo. Nimefanya hivi ili kuokoa usichana wangu’
Magreth alizungumza huku akiendelea kumshuhudia nabii Sanga jinsi anavyo tetemeka kwa hasira huku j wake akilala                                 ***
“Kila mtu avae bulletproof yake”
Rama D alitoa agizo hilo kabla ya kushuka kwenye gari lake. Wadogo zake wakafanya hivyo, kila mtu akashuka kwenye gari lake huku bunduki yake akiwa ameikoki kisawa sawa.
“Shukeni kwenye magri”
Mkuu wa kikosi cha polisi, aliwaamuru askari wake na wakatii. Wakashuka huku gari hizo mbili za askari zikiwa zime kaa sawa. Wakafungua milango ya gari hizo kwa ajili ya kuzuia risasi ambazo zimesha anza kungurumishwa kutoka kwa majambazi hao. Umbali wa mita hamsini walizopo, ziliweza kuwapa nafasi ya mapambano hayo kudumu kwa muda mrefu huku wote wakishambulia kwa kusubiriana.
“Mkuu wa namna hii hatuto weza kuwadhuru, tuna maliza tu risasi zetu”
“Inabidi wawekwe kati”
“Ndio mkuu, nimewasiliana na askari wengine, wapo njiani wana kuja wakitokea nyuma yao. Tukiwaweka kati nina imani tuna washinda”
“Kazi nzuri, hakikisheni muna tunza risasi zenu”
“Poa poa’
Askari wote wakaacha kushambulia na kuwafanya Rama D na wadogo zake kushangaa.
“Wana mpango gani mbona wameacha kutushambulia?”
Selemani aliuliza huku akichungulia jinsi askari walivyo jificha kwenye magari hayo.
“Sijajua kwa kweli”
Rama D alijibu huku jasho likimwagika usoni mwake. Siku zote Rama D na wadogo zake wamekuwa wakitekeleza kazi za utekaji wao kwa urahisi sana kwa maana hao wateja wao huwavamia kwa kustukiza. Ila leo wamekutana na kikosi cha askari ambao nao wana mafunzo ya hali ya juu.
“Fuc** wametuweka kati”
Selemani alizunugmza mara baada ya kuona gari nne zikija nyuma yao.
“Sisi tudili na hawa wa nyuma na wewe Abdalah dili na hawa wa mbele’
Rama D aligawa majukumu hayo kwa wadogo zake hao wawili walio salia. Wakaanza mashambulizi upya na kuwafanya askari wanao kuja kwa nyuma yao kusimamisha magari yao umbali kidogo na kuanza kujibu mapigano hayo. Askari hawakuwa wajinga wa kupoteza risasi zao kirahisi, jinsi Rama D na wadogo zake wanavyo mimina risasi pasipo mpangilio, kukawapa askari uvumilivu ambao wana imani kwamba ukifikia hatua fulani, basi wata imaliza vita hiyo kirahisi sana.
“Risasi zimekwisha”
Selemeni alizungumza huku akitazama bunduki yake inayo toa moshi mbele, kwani ameachia risasi nyingi sana na magazine nne alizo kuwa ana zibadilisha kila baada ya magazine moja kuisha, nazo zote zimekwisha.
“Kwenye gari lako kwani huna magazine?”
Abdalah D alimuuliza Selemani huku akimgeukia.
“Zimekwisha”
“Ohooo hata mimi hapa magazine yangu ina kwenda kuisha”
Abadlah alizungumza huku akisitisha kuwashambulia askari.
“Hata mimi nimeishiwa na risasi”
Kauli hizi zikaanza kuwaogopesha Rama D na wadogo zake. Kila mmoja matumaini yake ya kuishi tena yameanza kupotea taratibu. Abdalah akatoa magazine iliyopo kwenye bunduki yake na kukuta zikiwa zimebaki risasi tatu.
“Zimebaki risasi tatu na sina za ziada kaka”
Abdalah alizungumza kwa unyonge sana huku akikaa chini.
“Siwezi kukamatwa kijinga, tupigeni dua kisha tujiue. Mungu atatupokea vizuri”
Rama D alizungumza, wakashikana mikono wote watatu, wakaanza kusali dua hiyo huku wote wakiwa wamekaa chini. Dua hiyo haikuchukua dakika hata tatu tayari wakawa wamesha imaliza.
“Nitakuwa wa kwanza”
Rama D alizungumza huku akiichukua bunduki hiyo aina ya AK47 kutoka mikononi mwa Abdalah. Akajiwekea mdomo wa bunduki chini ya kidevu chake. Bila ya majadiliano, akaachia risasi moja ambayo haikufanya kosa zaidi ya kukifumua kichwa chake kwa juu.
Selemani D akamtazama mdogo wake Abdalah D anaye tokwa na machozi ya uchungu sana juu ya kushuhudia kaka yake akifa mbele ya macho yake. Woga wa Abadlah ukaanza kujidhihirisha usoni mwake na kumfanya Selemeni D kumtazama kwa sekunde kadhaa.
“Samahani Abdalah”
Selemeni D alizungumza na akampiga mdogo wake risasi ya kichwa na akapoteza maisha hapo hapo. Selemani D, akatoa kiberiti na pakti ya sigara mfukoni mwa suruli yake. Akatoa sigara moja na kuibana na lipsi zake, akaiwasha na akaanza kupiga mafumba mazito mazito, huku akishuhudia damu za ndugu zake jinsi zinavyo tapakaa kwenye barabara hiyo ya lami.
Selemani D akaivua bulletproof yake kisha akasimama huku bunduki hiyo akiwa ameishika mkononi mwake, akajitokeza kwa askari na akaachia risasi moja iliyo salia kwenye bunduki hiyo, huku akitambua nini kinakwenda kumpata.
    Askari wenye hasira kali sana na wenye uchu wa kuua wakaanza kuvurumisha risasi zisizo na idadi, kuelekea eneo alilo simama Selemani D. Hapakuwa na askari aliye piga risasi yake pembeni na risasi zote zikampata Selemeni D na kumuangusha chini huku mwili wake ukiwa umechakaa kwa kupigwa risasi hizo na huo ndio ukawa mwisho wa maisha yake.
Ukimya kutokea katika eneo zilipo gari za majambazi, zikawafanya askari kuanza kujitokeza kwenye magari yao huku wakianza kuzifwata gari hizo za majambazi kwa umakini sana. Wakamfikia Selemeani D na mmoja wa askari akaipiga teke bunduki iliyopo karibu na mwili wa Selemani D na kuifanya bunduki hiyo iserereke hadi pembezoni mwa barabara.
“Majambazi wote wame kufa”
Askari walianza kupeana ripoti huku wakikagua magari ya majambazi hao. Wakajikuta wakistushwa sana kwa kuto kumuona nabii Sanga katika eneo hilo.
“Nabii Sanga hayupo”
“Hayupo…………!!!?”
Mkuu wa kikosi hicho alizungumza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana, kwani lengo la oparesheni hiyo ni kumuokoa nabii Sanga na kuwaangamiza majambazi hao.
                                ***
“Yaani hawakuona sehemu ya kufanyia uchafu wao hadi kanisani kwangu tena ndani ya ofisi yangu?”
Nabii Sanga alizungumza huku akiwa ame fura kwa hasira.
“Ndio baba na hapo wamezungumzia juu ya kuniuua mimi”
Magreth alizungumza huku machozi yakimlenga lenga.
“Una MB humu ndani?”
“Ndio”
Nabii Sanga akajitumia video hiyo kwenye email yake, kisha akamrudisha Magreth simu yake. Akasimama na kujifunga taulo ambalo alilifungua kimakusudi.
“Baba naomba usitishe ule mpango wa kunifungulia mgahawa na kunipangishia nyumba. Wataniua kirahisi, nitaendelea kuishi maisha yangu ya kawaida na nitaendelea kuifanya biashara yangu ya kuuza maandazi baba. Kama Mungu hakunibariki kwa kupitia wewe basi ata nibariki kwa njiani nyingine.”
Magreth alizungumza huku machozi yakimwagika.
“Mage una ongea nini? Nitafanya kila kitu kwa ajili yako na kama yule mwana haramu Tomas wale jamaa zake watakuwa hawaja mfanya nilicho waagiza nita hakikisha kwamba nina muua kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Nabii Sanga alizungumza huku mwili mzima ukimtemeka kwa hasira. Leo hii amejua ubaya wa mke wake, si kuisaliti ndoa yao, bali amekwenda mbali sana hadi kupanga kumteka.
“Mke wako naye?”
“Nitadili naye ninavyo jua mimi. Ili kukuhakikishia kwamba sijabadilisha mawazo yangu ya kukusaidia, kesho kuki pambazuka, nitampigia simu muhasibu wangu aje hapa, mutaenda benki na utafungua akaunti yako na atakuingizia pesa nitakayo ihitaji mimi”
“Lakini baba, mke wako ata niua?”
“Achana na wasiwasi wa mke wangu. Niamini mimi, hembu njoo hapa”
Nabii Sanga alizungumza kwa kujiamini sana. Magreth akaka kitandani hapo huku wote wakibubujikwa na machozi.
“Hivi mwanamke kama huyu, katili, jambazi na ana analiwa hadi ***** kweli ana stahili kuwa mke wangu. Ana stahili kuendelea kuitwa mama mchungaji? Hapana siwezi kuishi na adui nyumba moja na sijapewa upako wa kumvumilia mtu wa namna hii Mage”


Nabii Sanga alilalama kwa uchungu sana hadi Magreth akajikuta akiingiwa na roho ya huruma.
“Mimi najichunga siku zote. Yeye kweli ni wa kunisaliti mimi. Ona jinsi kanisa linavyo muheshimu. Ona kila siku ninavyo simama madhabahuni mwa bwana na kukanya watu wasitende mabaya, wasitumie miili yao vibaya katika swala la mapenzi. Kumbe makatazo yangu ndio anayo yafanya mke wangu, ehehee?”
Nabii Sanga alizidi kulia kama mtoto mdogo. Taratibu Magreth akakilaza kichwa cha nabii Sanga katika bega lake la mkono wa kulia na kuanza kumbembeleza.
“Pole sana baba”
Nabii Sanga akayatupia macho yake kwenye kifua cha Magreth na akayaona maziwa ya mwanamke huyu anaye zidi kumchanganya na kumpagawisha. Taratibu nabii Sanga akaupeleka mkono wake wa kulia kifuani mwa Magreth na kushika z*wa lake moja, huku akijifanya ana endelea kulia. 


Kitendo hicho kikausisimua sana mwili wa Magreth, ikiwa ndio mara yake ya kwanza maishani mwake kukumbwa na hali hiyo. Magreth akajikuta akikaa kimya na kumfanya nabii Sanga azidi kulitomasa zwa hio la Magreth ambalo limenona kisawa sawa.

    Taratibu nabii Sanga akamlaza Magreth kitandani. Joto kali analo lihisi Magreth mwilini mwake, likamfanya azidi kuwa mpole huku akitamani joto hilo liweze kushushwa haraka. Nabii Sanga, akalifungua tenge la Magreth na akabaki kama alivyo .


Nabii Sanga alivyo hakikisha kwamba amesha mlegeza Magreth, taratibu aka.....
“Pole baby”


Nabii Sanga alizungumza huku akiendelea kuvunja ungo wa Magreth. 


Baada ya dakika kumi na tano za mwendo wa taratibu, nabii Sanga akajikuta akifika tamati huku jasho likimwagika mwili mzima. Ukimya ukatawala kati yao huku kila mmoja akitamani kumuanza mwenzake.
“Mage”
“Bee”


“Nina kupenda sana. Nina kuamini sana na nipo tayari kukufanyia kila kitu. Nitahakikisha kwamba una kuwa tajiri na umasikini una usahau. Umenielewa mama?”
“Ndio”


Magreth alijibu kwa sauti ya upole na iliyo jaa aibu kubwa sana. Hakutarajia siku hata moja kama atakuja kumkabidhi nabii Sanga mwili wake tena na bikra yake ambayo alikuwa akiitunza kwa ajili ya mwanaume atakaye muoa.


“Ila nina ombi moja. Endapo atatokea mwanaume akakuchukua mara ya mimi kukubadilisha kimaisha. Haki ya Mungu, nitamuua mbele yako na utashuhudia jinsi nitakavyo ufanya ukatili huo. Kwani sinto kuwa na huruma kabisa na yeye”


Maneno ya nabii SANGA yakamstua sana Magreth, kwani moyo wake haupo kabisa kwa nabii Sanga kwani mwanaume anaye mpenda kuliko kitu chochote ni Evans ambaye yupo hospitalini akipatiwa matibabu kwa pesa za nabii Sanga.


 ITAENDELEA
Haya sasa, nabii SANGA amesha jipatia utamu alio uhitaji kutoka kwa Magreth na kutoa onyo kali ikiwa moyo wa Magreth haupo kwake, je nabii Sanga ata fanikiwa kulinda penzi la Magreth lisivuje kwa Evans? Nini kitatokea? Endelea kufaatilia kisa hikii cha kusisimua, usikose sehemu ya 11.
 
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )