Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, July 29, 2020

Mwijaku afikishwa mahakamani akituhumiwa kusambaza picha za ngono

juu
Msanii wa uigizaji nchini Tanzania, Mwemba Burton (35) maarufu Mwijaku amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akituhumiwa kusambaza picha za ngon kinyume cha sheria
 
Mwinjaku ambaye alikuwa mmoja wa watia nia jimbo la Kawe, amefikishwa mahakamani hapo leo, Julai 29, 2020 na kusomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.
 
Akisomewa shtaka lake, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Mwanaamina Kombakono, alidai kuwa mshtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 110.
 
Wakili Kombakono alidai mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar Es salaam.
 
Alidia katika kipindi hicho, Mwijaku anadaiwa kuchapishwa picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliuounganishwa katika Kompyuta.
 
Mshtakiwa amekana shtaka na amekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kutoka ama Bongo Movie au tasnia ya muziki wenye barua zilizothibitishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), ambao watasiani bondi ya Sh  500,000 kila mmoja.
 
Hakimu Kabate ameahirisha Kesi hiyo hadi Agosti 12, 2020 itakapotajwa.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )