Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, September 28, 2020

Bashiru atoa Onyo kwa Wanaokusanya kadi za Wapiga kura kuwarubuni.

juu

Na John Walter- Manyara
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametoa onyo kali kwa wale wote wanaopita kukusanya shadada za kupigia kura kwa visingizio vya kutoa mikopo kwa wananchi.

Ametoa onyo hilo  Septemba 27, 2020 akiwa  kata ya Engusero wilaya ya  Kiteto Mkoa wa Manyara akiwa ameongozana  na Mgombea Mwenza wa CCM wa Urais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan  baada ya uzinduzi wa Kampeni awamu ya tatu kati ya sita, uliofanyika wilayani  Kongwa mkoa wa Dodoma.

"Tusilaghaiwe, shahada yetu ya kupiga kura, ina kazi ya kupiga kura tusidanganywe kwamba shahada hiyo unaweza ukapata mikopo, ukiona mtu anakwambia hivyo mtafute mwenyekiti wa Kitongoji akamatwe na achukuliwe hatua za sheria."

Katibu Mkuu ameongeza kuwa, "Ukiona mtu anakuhamasisha kufanya fujo, usimkubalie kwasababu nchi hii ni nchi huru na ni kisiwa cha amani."

Awali, katika uzinduzi huo, Wilayani Kongwa Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuzipongeza kamati za siasa za ngazi zote pamoja na wenyeviti wa mashina kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha ushindi mkubwa unapatikana.

Uzinduzi huo ni wa awamu ya tatu kati ya sita ambapo awamu ya nne itafanyika Zanzibar.
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )