Mlezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa
wa Manyara, Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mheshimiwa Mizengo Peter
Pinda amewataka watanzania waendelee kukiamini chama hicho kwa
kuwapigia kura Madiwani,Wabunge na Rais ifikapo Oktoba 28,2020.
Ameyazungumza
hayo Mjini Babati wakati akimnadi kwa wananchi wa mji huo mgombea
ubunge Paulina Gekul katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Papaa.
Amesema
Chama cha mapinduzi ni chama Kikongwe na kimefanya mambo mengi hivyo
ni vigumu kuondolewa madarakani kwa kuwa kimejidhatiti kujali maslahi
ya watu na utekelezaji wa kile wanachokiahidi.
Amesema yote
hayo yanafanyika katika mazingira ambayo ni tunu kwa Watanzania wote wa
Bara na Zanzibar katika hali ya amani na Utulivu ambavyo ni tunu kubwa
tangu kupatikana kwa uhuru na kwamba hakuna M'badala wake zaidi ya Chama
cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Pinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2020, ni Mratibu wa kamati za Kampeni katika mikoa ya
Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga.
Mgombea Ubunge Paulina
Gekul amesema serikali imefanya mengi katika Jimbo la Babati na kata
zake nane kwa kuleta maendeleo katika nyanja zote ikiwemo Elimu,Afya na
Miundo mbinu.
Amesema kupitia Serikali ya Chama cha Mapinduzi
Jimbo hilo kata zote zinapitika kwa kuwa bara bara zote zimechongwa na
TARURA na kamba katika kipindi kijacho cha awamu ya pili, wanatarajia
kupokea mradi mwingine wa lami zaidi ya kilomita 35 ambazo zitaondoa
vumbi katika mji huo.
Gekul amesema katika kukamilisha ujenzi
wa Miundo mbinu ya Mitaro na Vivuko katika mji wa Babati, wanajiandaa
kupokea zaidi ya shilingi Bilioni 10.4 ili kukabiliana na Mafuriko.
Akizungumzia
Mawasiliano, Gekul amesema serikali kupitia mtandao wa Halotel
wanajenga Minara ili vijiji vya Imbilili,Himiti,Chem Chem vilivyokuwa
havipati mawasiliano viweze kunufaika.
Kuhusu Ujenzi wa Kituo
kikuu cha Mabasi, Mgombea huyo amesema katika awamu ya pili kuanzia
mwezi Machi,2021 serikali imetenga Bajeti ya Shilingi Bilioni 12.7 kwa
ajili ya miradi ya Kimkakati.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )