Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, October 3, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump Apelekwa Hospitali Baada ya Kupata Corona

juu


Rais wa Marekani Donald Trump jana amepelekwa katika hospitali ya kijeshi kupatiwa matibabu baada ya kukutikana na ugonjwa wa Coreona.

Trump amehamishiwa katika hospitali ya Walter Reed saa 17 baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo. 

Katika vidio fupi aliyoituma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Trump ameonekana akisema kwamba hali yake inaendelea vizuri. 

Msemaji wa Ikulu ya White House Kayleigh McEnany amesema Trump atafanya kazi katika chumba maalum hospitalini kwa siku chache zijazo kama hatua ya tahadhari.

 Inasemekana kwamba Trump mwenye umri wa miaka 74, anasumbuliwa na homa na kwamba atapewa dawa ambayo bado inafanyiwa majaribio. 

Rais huyo wa Marekani wa chama cha Republican amepata ugonjwa wa Corona  akiwa katikati ya kampeni kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo atachuana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden.

 

-DW

ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )