Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 5, 2020

Mamlaka yaonya Watoa huduma za maji taka


 Samirah Yusuph
Maswa. Watoa huduma za maji taka katika wilaya ya Maswa wametakiwa kuzingatia usalama wa afya wawapo katika majuku yao kwa kuvaa vifaa maalum vinavyo weza kuwakinga na uchafu ili kujilinda na magongwa ya mlipuko.
Agizo hilo limetolewa na afisa afya wa wilaya hiyo Abel Machibya kufuatia uwepo wa wa wafanyakazi wanao toa huduma hizo bila ya kuwa na vifaa kazi kwa ajili ya usalama wa afya jambo ambalo ni hatari  na linaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa yanayosababishwa na uchafu.

Machibya alisema kuwa usalama wa usafi lazima uambatane na mazingira bora kwa wale wanaofanya kazi ya kutunza huduma  za usafi kwa kulinda afya zao na kuongeza kuwa:

"watu wote wanatoa huduma za usafi katika wilaya hiyo kabla ya kupatiwa kazi hizo hujaza mkataba na moja ya kipengere katika mkataba huo ni kila anayeomba kazi ya kufanya usafi ni lazima  ahakikishe usalama wa wafanyakazi wake kwa kuwa na vifaa kinga wakati wa kazi".

 Aidha alisisitiza iwapo wafanya usafi hawana vifaa kinga wakati wa kufanya kazi zao zikiwemo za kutapisha vyoo ni marufuku kufanya kazi hiyo na ikibainika wanafanya kazi katika mazingira hatarishi hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika wote kwani hali hii ikiachwa itaeneza magonjwa.

Hali iliyoelezwa na wafanyakazi hao kuwa mara nyingi hukaribiana na uchafu wa kinyesi cha binadamu, na hufanya kazi bila ya vifaa au kinga kwa kutumia mikono yao suala ambalo huwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa mengi.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wafanyakazi walioajiliwa na kampuni ya Mbiti walisema kuwa licha ya kutoa huduma hiyo muhimu katika jamii lakini viongozi wao waliowapa kazi hiyo hawajali afya zao pamoja na kuwa wanawaingizia fedha.

Walisema kuwa licha  ya kuomba kupatwa vifaa kinga wanapokuwa kwenye kazi zao lakini wasimamizi wao,wamekuwa wakiwapatia ahadi ambazo hazitekelezeki hali inayo wafanya wanaendelea kufanya kazi katika mazingira hayo hatarishi.

Ambapo hufanya kazi bila vifaa vya kuziba pua (Mask) na kuvaa mikononi (gloves) hali ambayo ni tishio kwa afya zao lakini  hiyo haijawa sababu ya wao kuacha kazi kwa sababu wanajitafutia kipato.
 
"Hii ndiyo hali yetu ya ufanyaji kazi siku zote sisi tumeajiliwa na kampuni ya usafi ya MBITI ambayo ndiyo imeingia mkataba na halmashauri ya Maswa kufanya usafi katika mji huu ikiwa ni pamoja na kutapisha vyoo vilivyojaa lakini hatupewi vifaa vya kujikinga kama ubavyoona,"alisema mmoja wa wafanyakazi ambaye hakutaka jina lake litajwe na kuongeza kuwa:

"Kazi hii ni ngumu kwani tunakumbana na kinyesi cha binadamu kwenye hivi vyoo bila tahadhari yoyote na afya zetu zipo hatarini kupata magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mlipuko na hata kwenye jamii tunaweza kupata magonjwa kama kipindupindu na kuhara hasa kipindi hiki cha msimu wa mvua"

Aidha wafanyakazi hao walitoa lawama kwa ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya ya Maswa kwa kutosikiliza kilio chao hicho licha ya kumjulisha kuwa wanahatarisha maisha yao kwa kufanya kazi bila vifaa kinga.

Akifafanua juu ya malalamiko hayo msimamizi wa kampuni hiyo Masanja Mbiti alisema kuwa malimbikizo ya madeni kutoka katika halmashauri yanapelekea kampuni hiyo kukosa fedha kwa ajili ya kununua vifaa kazi.

"Hata mie sipendi hawa wafanyakazi kufanya kazi bila vifaa kinga lakini nashindwa nifanyaje maana tunadai fedha za miezi sita hatujalipwa na halmashauri maana ndiyo tulioingia nao ubia wa kazi hii nikipata fedha nitanunua kama ilivyo kawaida nami nathamini afya za hao wafanyakazi wangu,"alisema.

Na kuongeza kuwa siku za nyuma alikuwa akinunua vifaa hivyo ambavyo ni mipira migumu ya kuvaa mikononi pamoja na barakoa kwa ajili ya wafanyakazi wake lakini sasa ni miezi sita hajalipwa fedha na halmashauri ya wilaya ya Maswa.

"Hata mie sipendi hawa wafanyakazi kufanya kazi bila vifaa kinga lakini nashindwa nifanyaje maana tunadai fedha za miezi sita hatujalipwa na halmashauri maana ndiyo tulioingia nao ubia wa kazi hii nikipata fedha nitanunua kama ilivyo kawaida nami nathamini afya za hao wafanyakazi wangu,"alisema.

Aidha alisema kuwa kuna wakati aliamua kutoendelea kufanya kazi hizo hadi hapo atakapolipwa fedha hizo lakini wafanyakazi hao waliamua kuendelea kazi bila  ya kuwa na vifaa kinga .

MWISHO
.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: